Nafasi Ya Matangazo

September 09, 2015



Huawei yaingiza sokoni simu mpya aina  ya Mate S
 -Itaanza kuuzwa kwenye soko la Tanzania mwezi ujao

Kampuni ya Huawei imeingiza sokoni simu mpya aina ya Huawei ate S ambayo ina mwonekano wa kuvutia pia imewekewa program mbalimbali za kisasa zinazotumia Android.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Huawei Richard Yu amesema kampuni  yake imejizatiti vya kutosha kwa kuhakikisha inaingiza sokoni bidhaa zenye ubora wa hali ya juu zinazoendana na wakati wa kisasa na  kukidhi matakwa ya wateja kwenye masoko  mbalimbali duniani.

“Lengo letu kubwa wakati wa kuifanyia ubunifu simu hii mpya hadi kuitengeneza ni kukidhi matakwa ya watumiaji wa simu zinazotumia interneti maarufu kama Smart Phone na kuiongezea vionjo mbambali ambavyo wateja wanahitaji na havipatikani katika simu zilizopo sokoni”.

Amesema pamoja na kuongezewa ubunifu na vionjo vya ziada vya kitekinolojia bado aimu hii utumiaji wake ni rahisi  umezingatia maoni ya watumiaji wa simu za Smart katika masoko mbalimbali.

Baadhi ya vionjo vya kiteknolojia kwenye simu hii ni kuweza kutoa tahadhari za papo kwa mtumiaji pia uwezo wake katika program za muziki ni mkubwa bila kusahau kamera inayotoa picha zenye mwonekano wa kiwango cha hali ya juu.

Simu hizi zinapatikana katika rangi mbalimbali kulingana  na mahitaji ya wateja kwenye masoko,zipo za rangi ya dhahabu,shaba.chuma na nyinginezo  nyingi za kuvutia bila kusahau umbo lake zuri.

Pia simu ya Huawei Mate S imetengenezwa kwa malighafi bora zinazokidhi viwango vya kimataifa zenye sifa ya uimara ambazo zinaifanya simu  kuweza kudumu kwa kipindi cha muda mrefu na sio rahisi kwa maharamia wa bidhaa kuigiza utengenezaji wake.

Sifa nyingine ya pekee ya simu hii ni kukaa na chaji kwa muda mrefu na internet wa haraka na kasi kubwa inayokidhi mahitaji ya wateja.

Kwa kuanzia simu hii itauzwa katika nchi zaidi ya 30 zikiwemo China,Ufaransa,Ujerumani,Israel,Japan,Afrika ya Kusini, Umoja wa Falme za Kiarabu .

Meneja Masoko na mauzo wa bidhaa za Huawei nchini Tanzania Samson Majwala amesema kuwa simu hii mpya itaanza kuuzwa nchini kuanzia  mwezi ujao na ana imani itakidhi haja ya wateja wanaotaka kutumia bidhaa  bora zinazoendana na ulimwengu wa kisasa.

Maelezo zaidi yanapatikana katika tovutia www.consumer.huawei.com
Posted by MROKI On Wednesday, September 09, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo