

Kundi hili la washiriki waliohitimu mafunzo mbali mbali linabeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, ukiwa ni mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano.

Mradi huu uliandikwa na kuandaliwa na kampuni ya SSC Consulting wakiwa ndio washauri wakuu wa mradi huu, hasa katika kuandaa Utaratibu na mipango yote ya mafunzo ya biashara na ujasiriamali. Mradi huu unadhaminiwa na kampuni ya Shear illusions kwa lengo la kuwajengea uwezo wanwake wa Kitanzania Kupitia Bidhaa bidhaa za Vipodozi vya LuvTouch Manjano kujisimamia na kujikita vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara kwa lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa Kitanzania.
Kila mshiriki amepewa mtaji wa bidhaa za LuvTouch Manjano, vitendea kazi kumuwezesha kuwapodoa wateja, mafunzo ya biashara na ujasiriamali na pia atapewa Business Coach na Mentor (Dada mshauri) ili kumuongoza katika safari hii ya mwaka mzima katika kujikita kwenye ujasiriamali. Tunawatakia kila la kheri kizazi kipya hiki cha wajasiriamali kina mama.



Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Muasisi wa Mradi aliouanzisha kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye Ujasiriamali.Mafunzo Chini ya Taasisi ya Manjano Foundation.Lengo la Mradi huo ni kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania Kupitia Bidhaa bidhaa za Vipodozi vya Luv touch Manjano kujisimamia na Kujikita Vizuri kwenye Biashara ya Vipodozi na kujua Mbinu Mbalimbali za Biashara kwa lengo la Kumjengea uwezo Mwanamke wa Kitanzania.

0 comments:
Post a Comment