Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akionyesha Tuzo Maalum aliyokabidhiwa na Profesa Joseph
Adaikalam (kulia) Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Chuo Kikuu cha Binary kilichoko Kuala Lumpur
nchini Malaysia na kushoto ni Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Sulochana
Nair tarehe 24.7.2015.
Mke wa Rais
Mama Salma Kikwete akimkabidhi Tuzo Maalum aliyokabidhiwa na Uongozi wa Chuo
Kikuu cha Binary kwa Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Mlima tarehe 24.7.2015.
Mwenyekiti
wa WAMA na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akishuhudia utiaji saini (MoU) wa fursa za Binary First Lady of
Tanzania Scholarship kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu Cha Binary. Wanaotia
saini ni Ndugu Daud Nassib, Katibu wa WAMA na Profesa Joseph Adaikalam,
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Mtendaji wa Chuo Kikuu cha Binary cha nchini
Malaysia tarehe 24.7.2015. Kupita makubaliano hayo Chuo Kukuu cha Binary kitatoa nafasi 10 za shahada za uzamili.
Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji Mkuu wa Chuo Kikuu cha Binary Profesa
Joseph Adaikalam akibadilishana hati za makubaliano (MoU) na Katibu wa Taasisi
ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Ndugu Daud Nassib mara baada ya kutiliana saini
makubaliano hayo huku Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishuhudia.
Baadhi ya
viongozi wa Chuo Kikuu cha Binary na wqageni waalikwa waliohudhuria sherehe ya
tuzo na utiaji saini ya Makubaliano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha
Binary tarehe 24.7.2015 huko Kuala Lumpur nchini Malaysia.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba mara baada ya kutunukiwa Tuzo Maalum ya “
CWL International Women of Excellency Award for Leadership’ na Chuo Kikuu cha
Binary kilichoko nchini Malaysia tarehe 24.7.2015.
0 comments:
Post a Comment