BARAZA
la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NDC), na Benki ya Posta Tanzania,
(TPB), wamesaini makubaliano ya ushirikiano wa kuwawezesha wanachama wa VCOBA
nchini. Benki TPB na NDC kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati ya baraza na benki hiyo, katika
kuwawezwesha wana VICOBA kiuchumi. Hafla hiyo ilifanyika leo Julai 14, 2015. kwenye ukumbi wa
wizara ya fedha jijin I Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi, (NEC), Beng’ Issa, (kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Benjki ya Posta,
Sabasaba Moshingi, (wapilia kulia), Rais wa VICOBA Endelevu Tanzania, Devota
Likokola, (wapili kushoto), Mwanasheria wa Benki ya Posta Tanzania, Mystica
Mapunda Ngongi, (wakwanza kulia), wakiwa wameshikana mikono baada ya benki hiyo
kutiliana saini makubaliano ya ushirikiano kati ya baraza na benki hiyo, katika
kuwawezwesha wana VICOBA kiuchumi. Hafla hiyo ilifanyika leo Julai 14, 2015. kwenye ukumbi wa
wizara ya fedha jijin I Dar es Salaam.
************
Akizungumza
wakati wa hafla ya kutiliana saini makubaliano nhayo kwenye ukumbi wa wizara ya
fedha jijini Dar es Salaam leo Julai 14, 2015, Katib u Mtendaji wa baraza hilo, Beng’ Issa,
alisema, Katika juhudi za kuwawezesha watanzania kiuchumi kupitia upatikanaji
wa mitaji na kuendeleza ujasirimali nchini, Serikali kupitia Sheria ya Taifa ya
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya mwaka 2004, ibara ya IV, sehemu ya 16 iliagiza
uanzishwaji wa Mfuko wa Taifa wa Uwezeshaji Mwanachi yaani ‘’Mwananchi
Empowerment Fund,”.
“Katika
kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa mitaji yenye gharama nafuu kwa
wajasiriamali nchini, Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi limesaini
hati za makubaliano na Benki ya Posta Tanzania katika kusimamia udhamini wa
mikopo yenye masharti nafuu kwa
makundi mbali mbali ya wajasiriamali nchini yanayokidhi masharti
husika.” Alisema Beng’i.
Mfuko
huu utakao simamiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ni pamoja
na kutoa fursa kwa wananchi katika makundi au mtu mmoja mmoja kupata mitaji ya
kuwekeza kwenye miradi ya kiuchumi kupitia mikopo ya moja kwa moja au udhamini
(direct lending or guarantee system).
Ili
kutimiza azama hiyo baraza limeamua kushirikiana na benki ya ;posta Tanzania
ambayo ina mtandao mpana, kutekeleza azma hiyo ambapo wananchama wa VICOBA,
watapata mikopo na mafunzo kutoka benki ya posata. Soma zaidi hapa
0 comments:
Post a Comment