kikosi cha baobab
Mchezaji wa timu ya soka wa waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa
fc), Martin Peter (jezi ya kijani kulia) akipambana na mmoja wa
wachezaji wa timu ya makipa, Ivo Mapunda.
Na Mwandishi wetu
TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini (Taswa
FC) Ijumaa hii itacheza mchezo maalum wa kirafiki dhidi ya timu ya wafanyakazi
wa shule ya sekondari ya Baobab ya Bagamoyo.
Mchezo huo umepangwa kuanza saa 10.00 jioni kwenye uwanja wa
shule ya sekondari ya Baobab na tmgeni rasmi atakuwa mkurgugenzi wa shule hiyo,
Hlafan Swai.
Mbali ya Swai, viongozi wengine wa shule hiyo watahudhuria
mechi hiyo maalum kwa ajili ya kuhamasisha michezo shuleni hapo.
Mwenyekiti wa Taswa FC, Majuto Omary amesema kuwa awali
walipanga kucheza mechi mbili, ya wanaume (mpira wa miguu) na wanawake
(netiboli), hata hivyo wachezaji wa Taswa Queens hawakuweza kuanza mazoezi na
hivyo kulazimika kufuta mechi hiyo.
Majuto alisema kuwa wamepokea maombi kutoka uongozi wa shule
hiyo na hasa baada ya kutoa mwanafunzi bora kitaifa katika mtihani wa kidato
cha nne, Nyakaho Marungu. Alisema kuwa wamehamasika kupata mwaliko huo ambapo
mechi hiyo itakuwa kama sehemu ya sherehe ya kufunga shule.
Baadhi ya wachezaji wa Taswa FC wakataokuwepo katika mechi
hiyo ni Ali Mkogwe, Wilbert Molandi, Salum Jaba, Deogratius “Super Deo”
Maganga, Julius Kihampa, Sweetbert
Lukonge, Elius Kambili, Zahoro Mlanzi, Frank Balile, Mwarami Seif, Saidi Seif,
Jose, Martin Peter, Athuman Jabir, Muhidi Sufiani na Jabir Johnson.
Baadhi ya wachezaji wa
timu ya wafanyakazi wa shule hiyo ni John Kanakamfumu, Herry Morris
(kocha wa timu ya wanafunzi), Renatus Kavishe, David Ntungi, Hadji Juma, Madata
Lubigisa, Athuman Tippo na wengineo.
“Huu ni mchezo wa kudumisha ushirikiano wetu kwani sisi ni
waandishi wa habari za michezo na pia ni wazazi, hivyo tunaweza kuwapeleka
watoto wetu kusoma kaika shule hiyo bora, hivyo nawaomba wachezaji wote wafike
kwa wingi ili kuona mechi hiyo ya aina yake,” alisema Majuto.
0 comments:
Post a Comment