Nafasi Ya Matangazo

March 19, 2015



Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Kabwe Zubeir Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), huenda muda si mrefu kuanzia sasa akalihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano ikiwa ni Hotuba ya kuaga na kung’atuka kushika wadhifa huo wa uwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Kigoma Kaskazini.

Zitto NI Mchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliingia Bungeni kwa mara ya Kwanza mwaka 2005 akiwakilisha wananchi wa Kigoma Kaskazini kupitia chama cha Chadema.

Ameamua kuachia wadhifa huo na huenda pamoja na uanachama wake wa Chadema kufuatia mgogoro wa kisiasa uliopo baina yake na uongozi wa Chadema. 

Machi 15 Kabwe Zitto aliwaaga wapiga kura wake wa Jimbo la Kigoma Kaskazini kuwa hatokuwa tena Mbunge wao baada ya uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.

“Ni wakati sasa wa kutoa nafasi kwa nguvu mpya kuongoza Jimbo letu. Kushika kijiti pale ninapoishia. Kurekebisha pale nilipokosea. Kuimarisha pale nilipofikia”…”Sitakuwa mbunge wenu baada ya Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba lakini nitaendelea kutetea maslahi ya Mkoa wa Kigoma na Taifa letu kwa njia nyingine”.

Zitto amekuwa Mwanachama wa Chadema kwa takribani mika 24 ambapo akiwa amejiunga angali bado kijana mdogo na alifanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali katika chama hadi Naibu Katibu Mkuu Bara.
Posted by MROKI On Thursday, March 19, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo