Mwenyekiti wa kikundi cha Upendo Family Group ,Faustine Mwanadago (kushoto)akimkabidhi msaada wa katoni ya
maji muuguzi mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru,Sifael
Masawe jana kikundi hicho kilipofanya ziara ya kutembelea wagonjwa
hospitalini hapo,jumla ya mashuka 300 na maji katoni 10 zenye thamani ya
zaidi ya sh,2 milioni zilikabidhiwa ,anayeshuhudia pembeni ni makamu
mwenyekiti wa kikundi hicho,Jasmine Kiure: Habari Picha:Moses Mashalla wa jamiiblog.co.tz/
Mwenyekiti
wa kikundi cha Upendo Family Group ,Faustine Mwanadago
(kushoto)akimkabidhi msaada wa mashuka na maji muuguzi mfawidhi wa
hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru,Sifael Masawe jana kikundi hicho
kilipofanya ziara ya kutembelea wagonjwa hospitalini hapo,jumla ya
mashuka 300 na maji katoni 10 zenye thamani ya zaidi ya sh,2 milioni
zilikabidhiwa ,anayeshuhudia pembeni ni makamu mwenyekiti wa kikundi
hicho,Jasmine Kiure.
*********
Hospitali
ya mkoa wa Arusha,Mt Meru inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mashuka ya
kujifunikia kwa ajili ya wagonjwa mbalimbali waliolazwa hospitalini
hapo hali ambayo imepelekea baadhi ya wagonjwa hao kulala bila
kujifunika nyakati za usiku.
Kwa sasa hospitali hiyo ina jumla ya vitanda 500 na mashuka 300 wakati wastani wa kitanda kimoja kinatakiwa kuwa na mashuka 8.
Akizungumza
na waaandishi wa habari mara baada ya kupokea msaada wa jumla ya
mashuka 100 na katoni kumi za maji kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa
hospitalini hapo,muuguzi mfawidhi wa hospitali hiyo,Sifael Masawe
alisema kuwa tatizo la uhaba wa fedha kutoka serikali kuu limechangia
kukosekana kwa huduma mbalimbali hospitalini hapo yakiwemo mashuka.
Alisema
kuwa kwa nyakati tofauti baadhi ya wagonjwa hushindwa kujifunika
mashuka nyakati za usiku kutokana na uhaba wa mashuka hayo na kuwataka
wadau mbalimbali mkoani Arusha kujitokeza kuokoa hali hiyo.
Akikabidhi
misaada ya mashuka na maji kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika wodi
wa akina mama hospitalini hapo ,mwenyekiti wa kikundi cha Upendo
Family,Faustine Mwandago alisema kwamba misaada hiyo imegharimu kiasi
cha zaidi ya sh,2 milioni.
Mwandago,alisema
kuwa lengo la kukabidhi misaada hiyo ni kuonyesha upendo kwa watu wenye
mahitaji mbalimbali sanjari na kulienzi jina la kikundi chao kwa
vitendo huku akiwataka wadau wengine kuwaunga mkono.
0 comments:
Post a Comment