Bweni lililowaka moto.
Wananchi na wanafunzi wa shule ya sekondari Idodi Iringa
wakishiriki kuzima moto katika bweni la wanafunzi wa kike
shuleni hapo amnbalo lilikuwa likiwaka moto leo asubuhi.
*********
MOTO
mkubwa ambao chanzo chake kinatajwa kuwa ni hitirafu ya umeme
umeteketeza bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Idodi
wilaya ya Iringa mkoani Iringa .
Tukio hilo limetokea muda wa saa 4 asubuhi leo wakati wanafunzi wakiwa madarasani wakiendelea na masomo.
Katika mahojiano na m,tandao wa matukio daima, Kamanda wa jeshi la Zimamoto Mkoani Iringa, Inspekta
Kennedy Komba alisema kuwa bweni hilo limeteketea lote na kuunguza mali
zilizoko katika bweni hilo na chache kuokolewa na wananchi waliowahi
kufika eneo la tukio kusaidia kuzima moto huo.
Alisema kuwa chanzo cha moto huo imesababishwa na hitalafu ya umeme na hakuna mwanafunzi yoyote aliyejeruhiwa na moto huo.
“Endapo tungepata taarifa mapema nina amini tungeweza kuokoa vitu vingi zaidi na kuwataka wananchi wasitegemee mtendaji au kiongozi apige simu katika kikosi cha kuzima moto kwani kila mtu ana haki ya kupiga simu 111 katika kitengo cha mawasiliano cha jeshi hilo kuweza kutoa taarifa ya majanga, tumetumia muda mdogo kufika eneo la tukio kutokana ubora wa gari hivyo nawashukuru sana wananchi kwa taarifa na kuweza kuonyesha ushirikiano katika uzimaji wa moto huo usilete madhara zaidi “ alisema
Akizungumzia hasara iliyosababishwa ni kiasi gani Komba alisema hadi sasa hawajapata tathmini kamili ya mali zilizoteketea ila baada ya kazi kukamilika itafahamika ni thamani ya vitu vilivyoungua na kuwekwa wazi kwa wanachi.
Agosti
25/ 2009 jumla ya wanafunzi 13 walipoteza maisha baada ya bweni
hilo kuteketea kwa moto na baadhi yao kujeruhiwa kwa ajali kama
hiyo ya moto ambayo kwa kipindi hicho moto huo ulisababishwa na
mshumaa.
0 comments:
Post a Comment