Msanii wa Bongo fleva nchini, Ali Kiba akiimba akapela moja ya
nyimbo zake wakati wa mkutano huo na wandishi wa habari (Hawapo
pichani), katika mkutano huo juu ya ushiriki wake kwenye tamasha hilo
linalotarajia kufanyika Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe, Zanzibar.
kushoto kwake, ni Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Busara Promotions, Simai Mohammed.
**********
Mkali wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba ametamba kukonga
nyoyo watu mbalimbali watakaojitokeza kwenye tamasha la 12 la Sauti za
Busara linalotarajia kufanyika, Februari 12 hadi 15, Ngome Kongwe,
Zanzubar.
Ali Kiba alieleza hayo leo Alhamisi,
Januari 29. wakati wa mkutano wa ulioandaliwa na Busara Promotions,
wandaaji wa tamasha hilo kubwa la Kimataifa linalofanya muziki wa
'Live', ambapo kwa mwaka huu zaidi ya wanamuziki na vikundi 37, watatoa
burudani kwenye tamasha hilo kwenye viunga vya Ngome Kongwe, Unguja,
Zanzibar.
Akizungumza mbele ya wandishi wa
habari, Ali Kiba alisema kwa sasa amejiandaa kutoa burudani ya aina na
ambayo itakonga nyoyo kwa watu wote watakaojitokeza kushuhudia tamasha
hilo.
"Hii itakuwa ni zawadi kwa watanzania
wote kunishuhudia nikiimba 'live' bila kutumia 'cd' kama wafanyavyo
wengine. Mimi ni mwanamuziki na nimesoma muziki hivyo nitapiga muziki wa
nguvu jukwaani" alisema Ali Kiba.
Na kuongeza
kuwa, kwa sasa yupo kwenye mazoezi ya muda mrefu wa kujifua na bendi
maalum kwa ajili ya shoo hiyo huku akitamba kuwa, yeye ni msanii kwani
muziki aliusomea na kujifunza huko nyuma alipokuwa katika Nyumba ya
kuibua vipaji THT, ambapo alijifunza vitu vingi ikiwemo kuimba muziki wa
bendi na 'live'.
Aidha, aliwaomba wapenzi na wadau wa muziki kujitokeza kwa wingikushuhudia tamasha hilo kwani wasanii mbalimbali wa ndani na nje watatoa burudani ya kipekee.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya Busara Promotion, wandaaji wa
tamasha hilo, Simai Mohammed, alisema tamasha limeweza kuongeza ajira na
uchumi wa Zanzibar kwani pia limeongeza fursa za utalii.
Kwa
upande wake, Meneja wa tamasha hilo, Journey Ramadhani, alisema
tamasha hilo limeweza kuongeza fursa kila mwaka ikiwemo kutoa ajira kwa
vijana wa kitanzania kwa asilimia 90, ambapo kwa mwaka huu wanatarajia
kuwa na watendaji kazi na wa kujitolewa watakolipwa katika kusaidia
tamasha hilo, zaidi ya watu 150.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Yusuf Mahmoud 'Dj Yusuf' alisema
tamasha hilo limeweza kuibua wasanii mbalimbali ikiwemo kujitangaza
kimataifa.
Aidha, Dj Yusuf alieleza kuwa,
tamasha la mwaka huu litaendana na kauli mbiu ya kuimiza Amani, pia
wameandaa tuzo maalum na zawadi maalum kwa wasanii wa Tanzania
watakaoshinda katika kutunga nyimbo za amani.
Mbali
na Ali Kiba, Wasanii wengine Isabel Novella kutoka Msumbiji, Ihhashi
Elimhlophe (Afrika Kusini), Tcheka (Cape Verde), Diabel Cissokho
(Senegal), Culture Musical Club (Zanzibar), Msafiri Zawose (Tanzania),
Aline Frazão (Angola), Tsiliva (Madagascar), Leo Mkanyia and the
Swahili Blues Band (Tanzania), Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta
(Zanzibar), Thaïs Diarra (Senegal / Mali / Uswisi), Liza Kamikazi
and band (Rwanda), Erik Aliana (Cameroon), Mpamanga (Madagascar),
Mgodro Group (Zanzibar), Rico Single & Swahili Vibes (Zanzibar),
Zee Town Sojaz (Zanzibar), Ifa Band (Tanzania) na wengine wengi.
Maelezo zaidi yanapatikana katika www.busaramusic.org
0 comments:
Post a Comment