Timu
ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ikiwa
ndani ya MV Liemba mara walipofika kujionea mandhari ya meli hiyo kongwe
duniani.
Nahodha
wa MV Liemba, Kapteni Mathew
Mwanjisi (Watatu kushoto) akitoa
maelezo kwa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume
ya Mipango. Na Saidi Mkabakuli, Kigoma.
Wakaguzi wa Miradi ya
Maendeleo toka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wamepata fursa adhimu ya
kutembelea meli kongwe kupita zote nchini, MV Liemba iliyo kwenye Ziwa
Tanganyika, mkoani Kigoma.
Wakizungumza mara
walipofika katika meli hiyo baadhi ya wakaguzi hao hawakuficha bashasha
waliyokuwa nayo mara baada ya kuingia ndani ya meli hiyo kongwe iliyo na umri
zaidi ya miaka 100.
Mmoja wa wakaguzi hao
Bibi Zena Hussein, alisema kuwa anajisikia furaha sana kuingia na kushuhudia
mandhari ya meli hiyo ya kihistoria nchini Tanzania.
“Nimefurahi sana kufika
leo hii kwenye meli hii yenye miaka zaidi ya 100, licha ya ukongwe wake bado
inaonekana imara na yenye uwezo wa kufanya kazi miaka mingi zaidi,” alisema.
MV Liemba ni meli ya
Kitanzania inayohudumia pwani za Ziwa Tanganyika. Ni chombo cha usafiri wa
majini chenye umri mkubwa kuliko kingine chochote nchini na kipo tangu mwaka
1914. Meli hii kama zilivyo meli ningine inasukumwa na injini ya diseli na ina
urefu wake ni mita 67, upana mita 10 na uzito wa tani 1500.
Kwa mujibu wa Nahodha wa
meli hiyo, Kapteni Mathew Mwanjisi, meli hiyo ina uwezzo wa kubeba abiria 600
na tani za mizigo 200.
“Katika daraja la kwanza
meli ina uwezo wa kubeba abiria 20, daraja la pili abiria 30 na daraja la tatu
abiria 550,” alisema.
Meli ya MV. Liemba
inamilikiwa na Kampuni ya MSCL na kusajiliwa na Mamlaka ya Usafiri Nchi Kavu na
Majini (SUMATRA) kwa namba ya usajili KP/P001. Meli hiyo ilijengwa katika
Bandari ya Kigoma mwaka 1913 na mjenzi kutoka Ujerumani kwa ajili ya
usafirishaji wa mizigo na abiria.
Mv. Liemba ilitengenezwa
nchini Ujerumani mwaka 1913 ikiwa ikiitwa kwa Kijerumani "Graf von
Goetzen" kwenye kiwanda cha meli cha Meyer huko Papenburg.
0 comments:
Post a Comment