Na Fadher Kidevu Blog
KIUNGO mshambuliaji wa Simba Raphael Kiongera,huenda akalikosa
pambano la watani wa jadi Simba na Yanga kutokana na maumivu makali ya goti.
Kiongera alipata maumivu hayo Jumapili iliyopita wakati timu yake ikicheza na Coastal Union katika
mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara uwanja wa taifa.
Daktari wa Simba Yassin Gembe,amesema vipimo
alivyofanyiwa mchezaji huyo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili
vimeonyesha tatizo hilo ni lamuda mrefu na litachukua wiki sita hadi miezi
miwili ili liweze kupona na mchezaji huyo kurudi uwanjani.
Kamati ya usajili ya Simba imekuwa na sinto
fahamu baada ya majibu ya vipimo hivyo kwa sababu mchezaji huyo hakufanyiwa
vipimo wakati akisajiliwa kutoka KCB inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya.
Kiongera aliingia uwanjani dakika ya 66,kuchukua
nafasi ya Mrundi Amisi Tambwe,lakini alilazimika kutolewa kwa machela dakika za
nyongeza baada ya kugongana na kipa wa Coastal Union Shabani Kado ambapo timu
hizo zilitoka sare kwa kufungana mabao 2-2.
0 comments:
Post a Comment