Nafasi Ya Matangazo

August 11, 2014

r1Wafanyakazi wa Kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha,wakiwa wanafurahia kikombe walichonyakua juzi mara baada ya kuibuka washindi wa kwanza  katika sekta ya mawasiliano na habari katika sherehe za nane nane kanda ya kaskazini jijini Arusha,aliyevalia suruali nyekundu Sarah Keiya
 *****
 
Kampuni ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha,imeibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza  katika Sekta ya Mawasiliano na habari baada ya kushindanishwa na makampuni mengeni katika maonyesho ya nane nane kwa ukanda wa kaskazini yaliyofanyika hivi karibuni katika viwanja vya themi jijini Arusha

Akiongelea ushindi huo jana,Meneja masoko wa kampuni hiyo Bi,Sarah Keiya alisema kuwa chanzo cha ushindi huo ni kutokana na timu nzuri aliyonayo ndiyo iliyopelekea wao kuibuka kidedea kwa kuwa wamekuwa wakifanya kazi kwa umoja na mshikamano wa hali ya juu

"Najivunia timu yangu ya nguvu  kwa kweli sisi wafanyakazi wa Redio 5 tunashirikiana sana na tunafanyakazi kwa ushirikiano pia ,nawapongerza sana na Tunamshukuru Mungu kwa kufanukisha ushindi wetu"alisema Keiya

Pia Meneja huyo  alimpongeza mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw.Robert Francis kwa kuwawezesha kwa hali na mali kufanikisha utendaji wao walipokuwa katika maonyesho hayo ya nane nane.
Posted by MROKI On Monday, August 11, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo