Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Six Telecoms Limited, Rashid Shamte akizungumza katika
uzinduzi wa mtandao wa Virtual Private Network (VPN) kwa kushirikiana na kampuni maarufu ya
mawasiliano duniani, Tata Communications. Mtandao wa VPN utawawezesha
wafanyabishara nchini kukamilisha shughuli zao za kibiashara hapa nchini bila
ya kuvuka mpaka.
Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Six Telecoms Limited, Rashid Shamte akizungumza katika
uzinduzi wa mtandao wa Virtual Private Network (VPN) kwa kushirikiana na kampuni maarufu ya
mawasiliano duniani, Tata Communications. Mtandao wa VPN utawawezesha
wafanyabishara nchini kukamilisha shughuli zao za kibiashara hapa nchini bila
ya kuvuka mpaka.
Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Six Telecoms Limited, Rashid Shamte akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mtandao wa Virtual Private Network
(VPN) kwa kushirikiana na kampuni maarufu ya mawasiliano duniani,kulia ni
mwakilishi wa kampuni ya Tata Communications kanda ya Afrika, Steven Van der
Linde.
Mwakilishi
wa kampuni ya Six Telecoms Limited, Daniel Seyoun akielezea mafanikio ya
kampuni yao katika sekta ya mawasiliano ya Tehama nchini na nini watanzania
watafaidika baada ya kuzindua mtandao mpya wa Virtual Private Network (VPN)
ambao imeingia nchini kwa mara ya kwanza. Kulia ni Mwakilishi Mkuu wa kampuni
ya Tata Communications Kanda ya Afrika, Steven Van der Linde.
*********
Na
Mwandishi wetu
KAMPUNI
ya Six Telecoms Limited kwa kushirikiana na kampuni inayongoza duniani ya
Mawasiliano, Tata Communications imezindua mtandao maalum wa mawasiliano
ujulikanao kwa jina la Virtual Private Network (VPN) ambayo itawawezesha
kampuni za sekta ya biashara kuanzisha na kumalilisha shughuli zao bila
kusafiri nje ya nchi.
Uzinduzi
huo ulifanyika jana jijini ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Six Telecoms Limited,
Rashid Shamte alisema hiyo ni fursa pekee kwa wafanyabiashara nchini kuepuka
gharama mbali mbali katika shughuli zao kupata faida.
Shamte
alisema kuwa kwa kupitia mtandao wa VPN, mfanyabishara anaweza kuwasiliana moja
kwa moja na mshirika wake wa nje kwa njia ya picha, sauti wameamua kuanzisha
mtandao huo ili kuwawezesha wafanyabiashara nchini kuongeza wigo wa biashara
zao kwani mpaka sasa zaidi ya nchi 400 duniani zinatumia mtandao wa VPN.
Alisema
kuwa mtandao huo umeingia nchini kwa mara ya kwanza na unapatikana kwa bei
nafuu na ni salama zaidi kulinganisha na mitandao mingine.
“Mtandao
wa VPN ni wa kisasa na ni salama, hakuna mtu anayeweza kuingilia mawasiliano
kutokana na ni wa haraka zaidi, tunafurahi kuwa kampuni ya kwanza ya Kitanzania
kuanzisha huduma hii nchini baada ya mtandao wetu wa internet wa Metro kuongeza
ufanisi wa sekta ya mawaliano ya tehama nchini na nchi nyingine duniani,”
alisema Shamte.
Mkurugenzi
wa Tata Communications Kanda ya Afrika, Steven Van der Linde alisema kuwa
wamefurahi kuingia makubaliano hayo na Six Telecoms Limited na kuwaomba
wafanyabiashara kujiunga na mtandao huo.
Linde alisema kuwa kampuni yao ambayo makao
yake makuu yapo nchini India, imejipatia sifa kubwa katika sekta ya mawasiliano
ya Tehama na ujio wao Tanzania ni kuboresha sekta hiyo ambayo ni kubwa duniani.
Alisema
kuwa kwa kupitia VPN ambayo ni imeleta mafanikio makubwa katika bara la Afrika,
Asia-Pasifiki, Amerika, Ulaya na India,
wafanyabiashara watapunguza gharama mbali mbali za uendeshaji wa biashara zao
kwani shughuli zote zitafanyika nchini na kukuza uchumi.
“Nimefurahi
kupata fursa hii ya kuwekeza hapa nchini kwa kushirikiana na Six Telecoms
Limited, hii ni fursa pekee kwa wafanyabiashara kuanza sura mpya na kisasa
katika shughuli zao,” alisema Linde.
0 comments:
Post a Comment