Nafasi Ya Matangazo

May 14, 2014



 chifu  Gilbert Isambe akiwa na vazi la kichifu

chifu  Gilbert Isambe akiwa anaongea na vyombo vya habari pembeni ni mratibu wa tamasha la Mtu kwao bi Janeth Jonas
Zaidi ya machifu 100 kutoka katika mikoa mbalimbali hapa nchini wanatarajia kuuthuria katika tamasha la mtu kwao linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi May 15  hadi 20 mwaka huu katika kiwanja cha kumbu ya sheikh Amri Abeid jijini hapa.
Akiongea na waandishi wa habari jijini hapa Mratibu wa tamasha hilo ambaye ni mkurenzi wa kampuni ya Utamaduni Traning L.T.D  Janeth Jonas alisema kuwa tamasha hilo litashirikisha machifu 120 kutoka katika mikoa mbalimbali na makabila mbalimbali ya hapa nchini.
Alibainisha kuwa nia  na dhumuni la kuandaa tamasha hili la mtamaduni wetu ni kuweza  kuuenzi utamaduni wa mtanzani ambapo ni kuanzia mavazi ya makabila mbalimbali,vyakula pamoja na ngoma  kutoka katika makabila yote hapa nchini.
“pia katika tamasha hili tumeamua kuwaita machifu mbalimbali l kutoka katika  makabila mbalimbali hapa nchini na baadhi ya mchifu ambao watauthuria ni pamoja na chifu kutoka oldmoshi ambaye yeye ameshawasili hapa Arusha kwaajili ya tamasha hili  Gerald Mandera  ,chifu Gilbert Rugal Isambe kutok a  kasulu  na wengine wengi wote watakuwepo”alisema Janeth
Aidha alisema kuwa katika tamasha hili kila mtu atapata fursa ya kuona ngoma kutoka katika makabila mbalimbali  pamoja na kuonja chakula cha kila aina cha makabila ya hapa nchini pamoja na nje ya nchi 
Alisema kuwa pia katika tamasha hili zaidi ya vikundi vya ngoma 100 vitatumbuiza pamoja na wasanii mbalimbali akiwepo msanii wa ngoma za utamaduni Mrisho mpoto,wema sepetu  ,kundi la weusi kutoka Arusha,Jambo Squards ,Dogo janja pamoja na msanii kutoka nchini Kenya Daniel  ole Sekuo.

 Naye mmoja wa machifu ambaye atauthuria tamasha hilo Chiefu Gerald Mandera kutoka oldmoshi alisema kuwa  waandaaji wamefanya jambo jema sana kuanda tamasha hili  kwani wao ndo wametambua uwepo wa machifu na wameona umuhimu wao mpaka wameamua kuwakusanya pamoja katika tamasha kama hili.

Alisema kuwa sasa ivi serekali nayo inawajibu wa kujipanga vilivyo na kutenga siku maalumu kwa ajili ya kufanya tamasha hili kama jinsi wenzetu kutoka katika nchi zingine wanavyo azimisha siku hii  katika tarehe hizi na mwezi huu kila mwaka.
Aidha alibainisha kuwa kuwakusanya watu mbalimbali kutoka katika tamaduni mbalimbali pamoja na makabila mbalimbali itasaidia kwani inaweza  kuwezesha hata nchi kupata vazi la taifa kwani makabila haya yate yanakuja yakiwa yamevaa vazi la ukabila wao na hii itakuwa fursa pekee ya kuweza  kuchagua vazi hasili la mtanzanzia.

“ni  aibu kubwa sana unakuta sisi kama watanzania hadi leo hii atuna vazi linaloweza kutuwakilisha sisi kama watanzania na ukiangalia wenzetu wa n je ya nchi  wanamav azi yao ya kiutamaduni ambao ukimuona tu mtu amevaa  unajua katoka katika kabila Fulani  ,naitanishangaza sana kuona mtu anauzarau utamaduni wake na anauweka mbele utamaduni wa kigeni “alisema chifu  Gilbert Isambe

Aidha alibainisha kuwa hii ni fursa ya watu kuja kujifunza mambo mbalimbali kwa vitendo ,akiwasihi wanafunzi wa shule mbalimbali pamoja na wanavyuo mbalimb ali kuja katika tamasha hili kushuhudia na kuwaona machifu ambao mud a mrefu walikuwa wanawasoma tu kwenye vitabu bila kuwaona moja kwa moja.
Posted by MROKI On Wednesday, May 14, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo