Mbunge wa jimbo la
Nzega Mkoani Tabora kupitia CCM, Hamis Kigwangala, ametanabaisha kuwa
anatafakari kama anaweza kugombea Urais kwenye uchaguzi mkuu ujao
kupitia chama cha mapinduzi CCM.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua fununu zilizo enea
kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikiibua mijadala
mara kwa mara inayomshawishi
kugombea Urais mwaka 2015, Dk. Kigwangala amesema anatafakari jambo
hilo zito na kuongeza kuwa muda utakapofika atayazingatia maoni ya
wananchi.
Akizungumzia
maelezo kwamba haoni kama ni hatari kwake kutangazwa mapema kwamba
anataka kuwa kugombea Urais ni kujipunguzia sifa katika chama chake, Dk.
Kigwangala alisema yeye hajatangaza kama anataka Urais na wala
hajamtuma mtu kuanza kumfanyia kampeni, kwani watanzania wanaongozwa na
katiba yenye Uhuru wa kujieleza na kutoa maoni, hivyo hayo ni mawazo yao
na wana haki ya kufanya hivyo na yeye binafsi hawezi kuwapinga.
Hivi
karibuni kumeibuka mijadala mizito kwenye
mitandao ya kijamii na baadhi ya wanaharakati kutengeneza vuguvugu la
kumshawishi Dk. Kigwangala kuchukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania ifikapo mwaka 2015.
Mijadala
hiyo mizito imeanzishwa katika mitandao ya Internet na simu za mkononi
walio ipachika jina "Citizens for Kigwangala" ambapo katika mijadala
hiyo wamekuwa wakishawishiana na kumwagia sifa Dk Kigwangala kwamba
ndiye kiongozi pekee anayefaa kuwakilisha chama cha Mapinduzi katika
uchaguzi mkuu ujao.
Baadhi ya vijana wamekuwa wakijadili kuwa Dk Kigwangala ndiye anayeweza kuleta upinzani wa kweli kwa vyama vya upinzani,
wakijenga hoja kuwa amekuwa na misimamo na uwezo wa kujieleza kwa ufasaha ndani ya vikao vya bunge.
Dk
Kigwangala ni mbunge wa jimbo la Nzega mkoani Tabora, mwenye taaluma ya
udaktari wa tiba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge
ya tawala za mikoa na serikali za mitaa.
0 comments:
Post a Comment