Na Mwandishi Wetu
Warembo 17 wamejitokeza
kushiriki katika shindano la kumtafuta Redds Miss Tabata 2014.
Mratibu wa shindano hilo, Joseph
Kapinga alisema jana kuwa warembo hao wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa
Da West Park kila siku kuanzia saa nane mchana.
Kapinga aliwataja warembo
waliojitokeza kuwania taji hilo kuwa ni Ester Frank Kiwambo (20),
Jemima Huruma Mawole (22), Badra S. Karuta (20), Mercy Mathias Kazula (19),
Lydia Charles (22), Agnes Tarimo (18),
Agnes Alex (20), Catrina Lawrence Idfonsi (20), Nuru Omary Athumani (19)
na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
Wengine ni Annatolia Raphael (21), Mary Henry (21), Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail
(20), Ester Wilson Mbayi (20), Ambasia
Lucy Mally (22) na Faudhia Hamisi (21).
Warembo hao wanafundishwa na Neema Mchaki, Pasilida Mandali na mcheza
shoo wa kiume maarufu nchini Bokilo.
Washindi watano kutoka Tabata
watafuzu kushiriki Redds Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Anayeshikilia taji la Miss
Tabata Dorice Mollel ambaye pia ni Miss Ilala.Miss Tabata inaandaliwa na
Bob Entertainment na Keen Arts.
0 comments:
Post a Comment