Nafasi Ya Matangazo

March 13, 2014


 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombe katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Samwel Sitta akinadi Sera zake kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya zoezi la Upigaji kura kwa nafasi hiyo Leo Mjini Dodoma.
 
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa akimpongeza Samuel Sitta kwa ushindi.
Kampeni za Sammuel Sitta nje ya ukumbi wa Bunge.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na aliyekuwa Mgombe katika nafasi ya Uenyekiti Bw. Hashim Rungwe akinadi Sera zake kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya zoezi la Upigaji kura kwa nafasi hiyo Leo Mjini Dodoma.
  Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakifuatilia sera za wagombea hao jana.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Bw. Edward Lowasa akiweka karatasi ya Kura yake ya Kumchagua Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba leo Mjini Dodoma 
Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Wakipiga Kura Kwa ajili ya Nafasi Ya Mwenyekiti wa Bunge Hilo Iliyokuwa Ikiwaniwa na Bw. Edward Lowasa na Bw. Hashim Rungwe leo Mjini Dodoma.
*******************
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba,ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki, Mh Samwel Sitta ameibuka kinara kwenye nafasi aliyowania ya kuwa Mwenyekiti wa kudumu wa Bunge Maalum la Katiba, baada kumbwaga mpinzani wake,Wakili wa Kujitengemea, Hashim Rungwe. 

Sitta ameibuka kinara na kuichukua nafasi hiyo ya kuwa Mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge hilo Maalum katika kinyang'anyiro cha uchaguzi huo uliofanyika leo jioni mjini Dodoma.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda, Mh Ameir Pandu Kificho, amekabidhi madaraka hayo kwa mwenyekiti mpya Samuel Sitta baada ya kumaliza rasmi muda wake wa kuliendesha bunge hilo leo. 

Jumla ya Kura zilizopigwa ni 563 na zilizoharibika ni 7,kufuatia idadi hiyo ya Kura Ndugu Hashim Rungwe amepata kura 69 na Mh.Samwel Sitta ameibuka na kura 487,kwa Matokeo hayo imetangazwa kuwa Mh.Samwel Sitta ndiye mshindi wa kuanza kupambana na misukosuko ya bunge hilo ambalo kwa sasa litaanza kuendeshwa kwa kanuni.
Posted by MROKI On Thursday, March 13, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo