Nafasi Ya Matangazo

March 20, 2014

Meneja wa kinywaji cha Redd's Original Victoria kimaro akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kuzinduliwa kwa mashindano ya Redd,s Miss Tanzania 2014
Mkurugenzi wa kampuni ya LINO International Hashi Lundenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya kuzinduliwa kwa mashindano ya Redd's Miss Tanzania 2014 katikakati ni meneja wa kinywaji cha Redd's Original Victoria Kimaro na mwisho ni Meneja Masoko wa kinywaji cha Redd's Original Vimal Vaghmaria.
 Baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria kwenye uzinduzi jijini Dar Es Salaam.
 *****
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original, pamoja na Kamati ya Miss Tanzania leo wamezindua rasmi kuanza kwa mchakato wa kumpata “Redds Miss Tanzania 2014/2015.

Akizungumzia Udhamini wa mashindano ya mwaka huu Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Bi. Victoria Kimaro alisema “Redds Original, ina furaha kubwa siku ya leo kutangaza udhamini wa mashindano ya kumsaka mrembo atakayemrithi Happines Watimanywa (Redds Miss Tanzania wa sasa).

Nina imani wote tunakumbuka kuwa mwaka 2012 Redds ilisaini mkataba na Lino International wa kudhamini mashindano haya maarufu na yenye hadhi yake hapa nchini kama mdhamini mkuu kwa kipindi cha miaka mitatu, yaani 2012 hadi 2014, hivyo huu ukiwa ni mwaka wetu wa tatu kwa mujibu wa mkataba, tunayo furaha kubwa kusema kuwa Redds Original imeweza kutoa mchango wake kwa jamii ya kitanzania, hususan tasnia hii ya Urembo.” Alisema Victoria

Akizungumzia udhamini wa kinywaji cha Redds Original, mkurugenzi mkuu wa Lino International Bw. Hashim Lundenga alisema; Lino International ina kila sababu ya kuipongeza Redds Original, kwani zaidi ya kuwa mdhamini mkuu kwa miaka mitatu kinywaji cha Redds kimekuwa mdau mkubwa wa mashindano haya kwa miaka mingi. Kwa niaba ya Lino International na wadau wa tasnia ya Urembo tunawapongeza sana Redds Original kwa imani yao kubwa na mashindano haya ambayo hakika sasa yanavutia zaidi.

 Tuna imani kubwa kuwa mwisho wa mkataba huu wa miaka mitatu sio mwisho wa mahusiano mazuri kati ya Lino International, wadau wa Urembo na kinywaji cha Redds Original.

Aidha nawataka waandaaji wote wa mashindano haya kuanzia ngazi za vitongoji hadi kanda kufanya maandalizi mazuri na pia kufanya taratibu kwa kuzingatia masharti yaliyopo katika mkataba na mdhamini wetu mkuu  kinywaji cha Redd’s pasipo kwenda kinyume.
 
Posted by MROKI On Thursday, March 20, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo