Wakati
harakati za kutafuta ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea zikizidi
kushika kasi na kuvunja rekodi ya kushirikisha mataifa mengi duniani, baadhi ya
takwimu kuhusu hali ya usalama wa safari za anga duniani zimezidi kuibuka na
kufungua macho ya wengi waliokuwa wakiamini kuwa tukio hili ni la kwanza na /
ama miongoni mwa machache kupata kutokea duniani.
Mtandao wa
Usalama wa safari za Anga ama Aviation Safety Network ilitoa orodha ya
ndege zilizopotea tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia.
Kwa mujibu
wa takwimu hizo, ndege 88 zimepotea tangu mwaka 1948, hivyo kufanya wastani wa
ndege zinazopotea na kutopatikana wala miili ya abiria kuwa 1.33 kwa mwaka.
Hii ni
sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA
kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila
Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii
ilikuwa ripoti ya Machi 22, 2014.
|
March 22, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment