Nafasi Ya Matangazo

March 20, 2014



 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya iliyopo jijini na Mkoa wa Mbeya, Magreth Haule, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya walimu, wafanyakazi na wanafunzi wa shule hiyo  kwa maofisa wa kampuni ya Simu ya Airtel mara baada ya kupokea msaada wa vitabu zaidi ya 200 vya masomo tofauti tofauti kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne jana. (katikati) ni Ofisa Masoko wa kampuni ya mtandao wa simu ya Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jonas Mmbaga na Ofisa Mauzo wa kampuni hiyo Mbeya Priscus Kimario.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mbeya iliyopo jijini na Mkoa wa Mbeya, Magreth Haule (kushoto) akikabidhiwa msaada wa Vitabu vya masomo tofauti tofauti jana kutoka kwa Ofisa Masoko wa kampuni ya simu ya Airtel Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jonas Mmbaga, (katikati) vitabu hivyo vilivyotolewa msaada na kampuni hiyo.
*******
Kampuni ya simu ya Airtel chini ya mradi wa shule yetu imetoa msaada wa vitabu  vyenye thamani ya takriban shilingi milioni 2 kwa shule ya sekondari ya Mbeya.

Makadhiano ya vitabu yameshuhudiwa na jumuiya nzima ya Shule yenye zaidi ya watu takribani 1365 wakiwemo wanafunzi, walimu na wafanyakazi wengine waliokusanyika kwa shauku ya kupokea vitabu hivyo ikichagizwa na kauli mbiu ya Airtel Baba lao.

Afisa Masoko wa kampuni hiyo Kanda ya Kusini, Jonas Mmbaga amesema “lengo la kutoa msaada huo ni kutekeleza azma ya kuendeleza ushirikiano na jamii katika Nyanja mbalimbali ikiwemo elimu ili kukuza taaluma mashuleni. Chini ya mpango wa shule yetu tumeweza kuzifikia shule mbalimbali nchini na leo tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari mbeya.


Mbaga alisema Vitabu hivi ni vya masomo ya sayansi vikiwemo vya Hisabati, Kemia, Fizikia, na Biolojia, kwa ajili ya  kidato cha kwanza hadi cha nne. Na tumeichagua shule ya Sekondari Mbeya ili kuwakilisha shule nyingine zilizopo mkoani Mbeya.

“Tunaahidi kuendelea kuzifikia shule nyingi zaidi mkoani hapa na mikoa ya jirani kupitia mpango wetu maalum wa shule yetu ambao ni endelevu uliodumu zaidi ya miaka 7 mpaka sasa.  Tuaamini kwa kujikita kwenye sekta ya elimu tunaendeleza ushirikaino wetu na serikali chini ya wizara ya elimu kusaidia kutatua changamoto zilizopo husasani ya vitabu mashuleni na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini”.aliongoza Mmbaga

Kwa upande wake Mkuu wa shule ya sekondari ya Mbeya Bi Magreth Haule alisema” Nawashukuru sana Airtel kwa msaada wa vitabu walioutoa shuleni hapa huu ni uthibitisho kuwa Airtel wapo karibu na jamii hasa katika kuendeleza sekta ya elimu. Msaada huu ni mchango mkubwa na ni changamoto kwa wanafunzi na walimu kuongeza juhudi katika kuhakikisha tunakuza kiwango cha elimu shuleni hapa. Tunaahidi kuvitumia vizuri vitabu hivi kwa manufaa ya wanafunzi na jamii nzima kwa ujumla

Nao Wanafunzi  Revina Florence, Denis Michael na Happy Mwaisengela kwa nyakati tofauti na kwa niaba ya wenzao wameipomgeza kampuni ya simu ya Airtel kwa msaada huo na kwamba vitabu hivyo vitachochea hamasa za wanafunzi kuongeza bidii katika masomo ili kufikia lengo lililokusudiwa.

Vitabu hivyo ni mwendelezo wa shughuli za huduma kwa jamii zinazotelewa na Airtel kupitia mradi maalumu wa Shule yetu unaoziwezesha shule mbalimbali kutapa vitabu vya ada na kiada, mpaka sasa shule zaidi ya 900 zimeshafaidika na mpango huu
Posted by MROKI On Thursday, March 20, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo