Tamasha la
mwanamke na akiba, ni tamasha la kwanza na la kipekee kabisa kuwahi kufanyika
hapa nchini Tanzania. Tamasha hili lina nia n a dhamira ya kutengenzeza ujuzi
na kumuelimisha mwanamke kuhusu kuweka akiba na kujitengenezea fursa
mbalimbali.
Tamasha litawaelimisha
wanawake namna tofauti za kuweka akiba, na mbinu mbalimbali za kujikimu.
Tamasha hili linakusudia kuwaelimisha wanawake umuhimu wa kuweka akiba, mbinu
tofauti za kuweka akiba na jinsi ya kukabiliana na changamoto mbalimbali katika
kujiwekea akiba.
Akiongea na
waandishi wa Habari jijini Dar es salaam leo, Mkurugenzi wa Angels Moment, Bi
Pamela Mathayo, alisema tamasha hili litahusisha maonesho mbalimbali ya bidhaa
za akina mama, na litahusisha mihadhara minne kutoka kwa wataalamu wa masuala ya
kibiashara na wajasiriamali. Ni fursa mojawapo kwa watakaohudhuria kujipatia
utaalamu na kupanua wigo wao kibiashara, aliongezea. Tamasha hili litafanyika
siku ya tarehe 19 mpaka 21 ya mwezi wa pili, katika ukumbi wa Dar live-Mbagala,
Dar es salaam.
“Mgeni wa
heshima anatrajiwa kuwa mke wa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muugano wa
Tanzania, Mama Aisha Bilal. Tamasha hili litahudhuriwa na waonesha bidhaa
wapatoa 50, na zaidi ya watu 5000 wanatarajiwa kuhudhuria tamasha hili,
aliongezea Bi Pamela Mathayo.
Naye Meneja mawasiliano wa Angel Moments,
waandaji wa tamasha hilo alisema nia ya tamasha hilo ni Kuboresha
kasumba ya kujiwekea akiba, hususan ikwa akina mama, na mbinu mbalimbali za
kujiongezea kipatoKuongeza idadi ya wanawake katika mifuko mbalimbali ya akiba Kuwafunza
wanawake namna ya kujinufaisha na akiba zao, ama kwa muda mfupi , wa kati na
muda mrefu Kuwatoa wanawake katika utegemezi na umaskini kwa kuongeza kipato
chao Kujifunza kutoka kwa wanawake wengine ambao wamefanikiwa kutokana na
kuweka akiba Kungamua na kutengeneza midahalo ambayo itakua ni chachu ya
kuboresha uwekaji na uelimishaji wa kuweka akiba kwa mwanamke Kuwaleta pamoja
wadau mbalimmbali ili kusaidia kumkomboa mwanamke, hususani katika suala la
kuweka akiba Kutoa fursa kwa wafadhili kujitangaza, kutangaza bidhaa zao, na
pia kuwafikia watanzania wengi zaidi.
Tamasha hili limedhaminiwa na Said Salim
Bakhressa, NSSF, PPF, SSRA, UTT, National Housing Corporporation (NHC), Montage
Limited, CRDB, Ashton Media
0 comments:
Post a Comment