Makamu mwenyekiti taifa wa
chama cha mapinduzi (CCM) Phillip Mangula amewataka viongozi wa matawi
kusimamia ipasavyo kanuni za uchaguzi na uongozi na maadili wa chama hicho kwa
kupiga vita rushwa hasa kuelekea katika chaguzi za serikali za mitaa zinatarajiwa
kufanyika mwaka huu.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini
Dar es salaam katika salama za mwaka wakati akizungumza na wajumbe wa
halmashauri kuu ya tawi la ofisi ndogo za chama hicho lilipo Mtaa wa Lumumba.
Amewataka viongozi hao kuweka misingi
mizuri ambayo itawezesha kupatikana viongozi wazuri ambao hawatokani na mianya
ya rushwa ili kuwa na dira nzuri kuelekea katika uchaguzi Mkuu utakaofanyika
2015.
“Nataka kanuni za uchaguzi na
uongozi na maadili ziheshimiwe ili kupata viongozi ambao hawatatokana na
rushwa, na hakikisheni katika vikao vyenu vya chama mnasimamia agenda mbili
ambayo ni uchaguzi na kujadili mwenendo wa katiba mpya”
“Mkifualia hatua moja hadi
nyingine katika mchakato wa kuipata katiba kuanzia ushiriki wa wajumbe wa bunge
maalum hadi katika mjadala wa wajumbe wakipitia kifungu kimoja hadi kingine
mtakuwa na nafasi kubwa ya kutoa maoni yenu pale itakaporudi kwa
wananchi,”alisema Mangulla.
Akizungumzia uwepo wa serikali
tatu katika rasimu ya katiba mpya, Mangula amesema bado ni mapema mno
kuzungumzia hatia ya suala hilo kwani mchakato wa kuipata katiba bado mrefu
ambao mbali na wawakilishi wa bunge maalumu la katiba utashirikisha tena
wananchi ambao watapiga kura yao ya mwisho.
Mbali na kuwapongeza tume ya
katiba mpya kwa kufanya kazi kwa uwazi, amewapongeza wanachama wa ccm kwa jinsi
walivyoshirikia ama mmoja mmoja au katika kundi katika kuhakikisha wanatoa
maoni yao katika rasimu ya katiba ambayo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete
mwishoni mwa mwaka jana.
0 comments:
Post a Comment