TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la Habari Tanzania (MCT)
kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari
Tanzania(EJAT) 2013, imeongeza muda wa kuwasilisha kazi za kushindaniwa hadi
Januari 21, 2014.Tarehe ya awali ya kuwasilisha kazi hiyo ilikuwa Januari 15,
2014.
Muda huo wa kuwasilisha kazi
umeongezwa baada ya kuwepo kwa siku za mapumziko zilizofuatana na ofisi
kufungwa, jambo lililowafanya baadhi ya
waandishi washindwe kuwasilisha kazi zao kwa wakati. Vile vile hii ni
fursa nyingine kwa waandishi wanaotaka kushiriki kwenye EJAT2013. Hata hivyo
baada ya Januari 21, 2014 hakuna muda
zaidi utakaoongezwa.
Kamati ya Maandalizi ya EJAT 2013 inaundwa na
Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania
(TMF), Johns Hopkins University, Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini Mwa Afrika
–Tawi la Tanzania (MISA-Tan), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania
(TAMWA), Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Chama cha
Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), Jukwaa la Wahariri (TEF), HakiElimu,
AMREF, ANSAF, BEST-AC, SIKIKA, Chama cha Waandishi wa Habari Dhidi ya Ukimwi ( AJAAT)
na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya
Habari Tanzania (MOAT).
Kajubi D. Mukajanga
Mwenyekiti Kamati ya Maandalizi
ya EJAT 2013
0 comments:
Post a Comment