Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania
(TBS), Charles Ekerege na binti yake
wakiondoka katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam
jana kusikiliza mwenendo wa kesi yake ya matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa asilimia 50 ya punguzo la tozo ya
utawala kwa Kampuni mbili na kulisababishia TBS hasara ya Dola 42,543 za
Kimarekani.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania
(TBS), Charles Ekerege (kulia) na familia yake akitoka katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana kusikiliza mwenendo wa kesi yake ya
matumizi mabaya ya madaraka kwa kutoa
asilimia 50 ya punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili na kulisababishia
TBS hasara ya Dola 42,543 za Kimarekani.
**********
MASHAHIDI
wa Jamhuri katika kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la
Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekerege (pichani) ya matumizi mabaya ya
madaraka kwa
kutoa asilimia 50 ya punguzo la tozo ya utawala kwa Kampuni mbili na
kulisababishia TBS hasara ya Dola 42,543 za Kimarekani, wamedai kwa
nyakati tofauti kwamba mshtakiwa alitoa msamaha huo bila kibali cha
Baraza la Utendaji (kwa sasa Bodi ya Wakurugenzi).
Mashahidi
hao wa kwanza Mwansheria Batista Bitao na wa pili ni Mhandisi Joshua
Katabwa walitoa ushahidi huo mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando
anayesikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini
Dar es Salaam.
Akiongozwa
na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(Takukuru), Janeth Machulya shahidi huyo alidai kuwa katika kipindi cha
mwaka 2007 na 2009, kwa mujibu wa mikataba ya TBS na Kampuni ya Jaffar
Mohamed Ali Garage ya nchini Dubai na Quality Motors ya Hongkong
walipaswa kulilipa shirika hilo asilimia 25 baada ya kufanya ukaguzi.
Alidai
kuwa kati ya mwaka 2007 na 2009, Baraza la Utendaji (kwa sasa Bodi ya
Wakurugenzi) ni chombo pekee chenye dhamana ya kusimamia shirika hilo.
“Mwaka
2007 na 2009 nilikuwa naalikwa katika baraza la utendaji (Bodi ya
Wakirugenzi) lakini hatukuwahi kujadili suala la kusitisha tozo ya ada
ya utawala… suala hilo liliibuka mwaka 2011 baada ya menejimenti
kuwasilisha taarifa ya kutolewa msamaha kwa kampuni hizo mbili na
iliambatanisha na maelezo ya kuomba radhi kuhusu kosa la kutoa msamaha
huo bila kibali cha baraza hilo na kwamba halitajirudia,” alidai Bitao.
Akifafanua
zaidi alidai kuwa baraza hilo lilitoa maelezo yake kwamba kosa hilo
sijirudie tena na kwamba menejimenti baada ya kupitia maombi hayo
ilipaswa kuyawasilisha katika baraza hilo ili liweze kutoa uamuzi wa
kukubali au la.
Naye
shahidi wa pili, Katabwa alidai kuwa kampuni hizo ziliingia mkataba na
shirika lake kwa mkataba wa kulilipa asilimia 25 na kampuni hizo kubaki
na asilimia 75 kama wakala wao.
Alidai kuwa Machi 28, mwaka 2008 aliagizwa na aliyekuwa Mkurugenzi wa
TBS (wakati huo, Ekerege) kuandaa barua ya kutoa msamaha wa asilimia 50
kwa kampuni ya Jaffar Mohamed Ali Garage.
“Ekerege
aliniagiza niandae barua ya kuwakubalia msamaha huo na aliisaini tarehe
hiyo waliyowasilisha maombi yao… utaratibu huo ulitumika kwa kampuni ya
Quality Motors kupokea majibu ya msamaha huo” alidai Katabwa.
Katika
kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa Machi 28 mwaka 2008 na Agosti 7, mwaka
2009, katika ofisi za TBS iliyopo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam, kwa nia ovu Ekerege alitumia madaraka yake vibaya.
Ilidaiwa
kuwa mshtakiwa huyo alitumia madaraka yake vibaya kwa kutoa punguzo la
asilimia 50 ya ada ya utawala kwa kampuni hizo bila idhini ya baraza la
utendaji la TBS kinyume cha sheria namba 2 kifungu kidogo cha (3) ya TBS
ya mwaka 2005.
Ilidaiwa
kuwa kitendo hicho kiliziongezea kampuni hizo faida ya Dola 42,543 za
Kimarekani sawa na (kwa wakati huo) Sh. Milioni 68,068,800.
Upande
huo wa Jamhuri ulidaiwa shitaka la pili, katika tarehe na mahali pa
tukio la kwanza, mshtakiwa alilisababishia shirika kupata hasara ya
fedha hizo.
Mshtakiwa
alikana mashitaka yote mawili na yuko nje kwa dhamana na kesi hiyo
itaendelea kusikilizwa mfululizo Februari 5,6 na 7, mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment