Karani
wa fedha wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Leah Amani (kulia) ambaye
amehitimu Shahada ya Uzamili katika Sayansi (Uhasibu na Fedha) akipongezana na
mhitimu mwenzake wa Shahada ya Uzamili katika Utawala wa Umma, ambaye pia ni
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Angela Kiziga wakati wa mahafali ya 12 ya
Chuo Kikuu Mzumbe tawi la Dar es Salaam jana.
Baadhi ya wahitimu wakiwa bize na simu zao jana kabla ya kuanza kwa mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa Chuo
Kikuu Mzumbe, Prof. Joseph Kuzilwa (wa pili kulia) akiwa pamoja na Naibu Makamu
Mkuu wa chuo hicho, Prof. Josephat Itika (wa pili kushoto) na Kaimu Mkuu wa
Chuo, Prof. Daniel Mkude (kulia) wakati wa mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Mzumbe,
Kampasi ya Dar es Salaam jana. Kushoto
ni Bw. Ludovick Utoh ambaye ni Rais wa Baraza la wahitimu Chuo Kikuu Mzumbe.
Baadhi ya wahitimu
katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi ya Dar es Salaam jana. Katika mahafali hayo, jumla ya wahitimu 1225
walipata shahada za uzamili katika makundi nane ya programu mbalimbali.
Margareth Simalenga, akipozi kwa picha mara baada ya kuhitimu shahada ya uzamili katika Uongozi wa biashara (usimamizi wa mashirika) yaani Master in Business Administration (Corporate Management) katika mahafali ya 12 ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Cumpas ya Dar es salaam yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment