WILFRED NOEL KITUNDU
MWENYEKITI CHADEMA MKOA
SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013
KATIBU WA CHADEMA MKOA
S.L.P 260
SINGIDA
YAH: - KUJIUZURU UENYEKITI
MKOA SINGIDA
Somo hapo lahusika,
Ninapenda kukuarifu kuwa
nimeamua kujiuuzuru nafasi yangu ya uenyekiti wa mkoa ambayo nimekuwa
nikiitumikia kwa kipindi kirefu sasa kama kielelezo cha kuamini na kudai
demokrasia ya kweli ndani ya chama.
Ikumbukwe kwamba mimi ndio
mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mwanachama wa
300 kitaifa, hiyo ni heshima kubwa sana kwangu na sipo tayari kuipoteza kwa
kukubali kuwa sehemu ya udharirishaji huu wa demokrasia uliopitiliza
Maamuzi na vitendo
vinavyoendelea ndani ya chama chetu kwa sasa ni ubakaji na udharirishaji wa
demokrasia ya kweli tunayoihubiri mbele ya umma.
Kwa barua hii basi,
nimeonelea bora upate ufahamu huo kuwa si vema mimi kuendelea kupingana na
dhamira yangu inayonituma kuwa mwanademokrasia wa kweli.
Kwa kipindi hiki kifupi
mnaweza mkaendelea kuitumia anuani yangu ya posta mpaka hapo mtakapopata anuani
yenu tayari.
Ninatanguliza shukrani
zangu za dhati kwa wanachadema wote wanaopinga upuuzi huu uliofanywa na kamati
kuu ya chama.
Kusimamia haki, katiba na
misingi ya chama ni wajibu wangu, hivyo kwa namna yoyote ile sitaweza kuwa
tayari kufumba macho pindi ujinga wa namna hii unapoendelea kutekelezwa kwa
uwoga wa uchaguzi.
Nakutakia kila la heri
kwenye majukumu yako.
………………………………………………….
Wilfred N. Kitundu
MSIMAMO WA MWENYEKITI
CHADEMA MKOA WA SINGIDA DHIDI YA UAMUZI WA KAMATI KUU YA CHAMA
UTANGULIZI
Ikumbukwe kwamba mimi ndio
mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa SINGIDA na ni mtu wa 300
kitaifa kujiunga na Chama hiki. Nimejiunga mwaka 1992 siku ya mkutano mkuu kwanza
wa uzinduzi chama uliofanyika mnazi mmoja.
Nimekuwa nikijitolea vya
kutosha nguvu, muda na akili zangu nyingi kukijenga na kukilinda chama hiki
mpaka sasa mkoa wetu wa singida umepata wabunge watatu mmoja wa kuchaguliwa na
wawili wa viti maalum.
Tangu mwaka 1992 mpaka 2011,
chadema imekuwa ikitumia nyumba yangu kama ofisi, nimekuwa nikifanya hivyo kama
kielelezo change cha kudai na kupigania demokrasia ya kweli ndani ya nchi kwa
kuijenga CHADEMA imara.
Kwa kipindi chote hicho
nimekubali kujibana na kuipunja familia yangu stahili zake ili chama chetu
kikue kwa kasi mkoani kwetu, nashukuru mungu wanasingida waliitikia ombi nletu
na kutufuta majozi yaliyotokana na jasho langu kwa kutupatia mbunge mwaka 2010.
Hivyo nimehudhunika sana
kwa kitendo kilichofanywa na wajumbe wa kamati kuu cha kukiuka utaratibu na
kujivalisha mamlaka yasiyowahusu.
HISTORIA YA USALITI KWENYE
CHADEMA
Viongozi wa chama chetu
wamekuwa na historian a tabia ya kutubadilishia wasaliti na kuwapachika kila
aina ya shutuma kila kunapokaribia uchaguzi ndani ya chama.
Tuliambiwa na kuaminishwa
kuwa KABURU ni msaliti mkubwa ndani ya chama.
Tukaambiwa na kuaminishwa
kuwa CHACHA WANGWE alikuwa msaliti, tukafanyishwa vikao vya ndani,
tukaanzishiwa mikakati mbali mbali kuwa wangwe ni msaliti na kwamba anatumika.
WANGWE alipofariki hali
ikatulia kidogo, tukaanza kuimba na kumsifia kwamba ni kamanda, tukamuita
majina yote ya kishujaa lakini haikuwa na faida yoyote.
Sasa hivi tumeanza
kuaminishwa wasaliti wengine wapya, safari hii wasaliti hawa wamevuka usaliti
na kuwa WAHAINI, masikitiko yangu ni hawa wahaini ndio wale wale wengine
waliokuwa wakikitetea chama kipindi kinapingwa na waliokuwa wasaliti.
Bahati mbaya sana na cha
kufurahisha kama si cha kusikitisha hakujawahi kutokea Msaliti, Mhaini Wala
kiongozi yeyote anayetuhumiwa kukihujumu chama mwenye asili ya KILIMANJARO ama
KASKAZINI kwa ujumla, wahaini na wasaliti wote wanatokea mikoa yetu sisi
wanyonge.
WAVAMIZI NDANI YA CHAMA
Bahati mbaya sana,
harakati hizi za kuibua na kuwashuhulikia hawa wanaoitwa wasaliti zinafanywa na
wavamizi ama wahamiaji ndani ya chama, nitatoa mifano michache muda huu.
1. GODBLESS LEMA tulimpokea kwenye chama hiki mwaka
2009 akitokea TLP aliposhindwa kufanya siasa za ushindani baada ya kushiriki
kukiua chama hicho, lema alikwenda TLP akitokea NCCR-mageuzi aliposhindwa
kutimiza malengo yake ya kisiasa na kushuhudia akikiua chama hicho. Leo LEMA
ndio mpambanaji mkuu dhidi ya Zitto Kabwe, Dokta Kitila mkumbo na demokrasia ya
kweli ndani ya chama chetu, anaambatana na kijana mwengine anaitwa MAWAZO, huyu
wakati sisi tunapambana na CCM mwaka 2010 kuwanadi wagombea wetu wa ubunge
urais na udiwani, yeye alikuwa anagombea udiwani kupitia CCM tuliyokuwa
tunaipinga, ameingia chadema na sasa wale waliokuwa wanampinga akiwa huko leo
anawaita WASALITI na WAHAINI.
2. MCH. MSIGWA naye huyu ni hivyo hivyo tulimpokea
CHADEMA baada ya kushindwa na kuigombanisha NCCR na baadae TLP. Baada ya
kuvimaliza vyama hivyo sasa wamehamia chadema kutugombanisha na kutuharibia
chama chetu kwa makusudi kabisa.
3. Wengine vinara kwenye mgogoro huu ni Tundu Lissu,
bensoni kigaila, john mrema na wengineo hawa ni vijana tuliowapokea kuja
kujenga chama na sio kukibomoa chama kama wanavyofanya
4. TUNDU LISSU yeye ni kinara sana wa kumshambulia zitto
kwenye hili, lakini ninasikitika kusema kuwa Tangu nimekuwa mwanachadema na
Tangu nimemfahamu Lissu alipohamia CHADEMA hajawahi kufanya mkutano hata mmoja
wa kujenga chama ndani ya mkoa wa SINGIDA ukiondoa jimboni kwake. Tumemuona
Zitto akitoka bungeni na mara nyingine hata kigoma kuja kufanya mikitunano
maeneo mbali mbali hapa singida ikiwemo iramba, singida mjini na kwingineko, na
mtakumbuka zitto amewahi kukamatwa na polisi mkoni singida akikinadi chama,
hakuwa lissu. Sasa leo anapotoka mbele na kujinadi kuwa ana mapenzi mazuri na
chama kushinda zitto kabwe ni upuuzi unaopaswa kukemewa kwa nguvu kubwa sana.
Ninasikitika sana kuona
Mwenyekiti Mbowe na Katibu mkuu Slaa wanawakumbatia hawa, ninashangaa sana
kuona viongozi hawa wanakubali kuwa sehemu ya ubakaji huu mkubwa wa demokrasia.
Ninaamini kabisa vijana
hawa wanatumiwa na mwenyekiti na katibu mkuu kuutumia uzoefu wao walioutumia
kwenye vyama vyao vya awali mpaka kuviua.
KUHUSU KAMATI KUU NA
MAAMUZI YAKE.
Uamuzi wa kuwavua nyadhifa
zitto kabwe na wenzake kwa madai ya kuwa na mkakati wa siri wa uchaguzi, ni
uamuzi wa kipuuzi na wa kupuuzwa, kwenye hili kamati kuu imedhihirisha namna
gani inaundwa na watu wasio na weledi na hawaongozwi na misingi na taratibu za
chama.
Katika chama chochote
kile, kamati kuu haiwezi kuwa mshitaki mkuu, hiyo hiyo iwe mwendesha mashitaka,
hiyo hiyo iwe shahidi, hiyo hiyo iwe hakiku na hiyo hiyo iwe muandika hukumu.
Hapa wamedhihirisha ni namna gani wanaongozwa na Hisia na chuki zinazotawaliwa
na hofu ya uchaguzi ndani ya chama.
Kamati kuu hii ya sasa
haipo kwa ajili ya maslahi ya wanachama na chama kwa ujumla, ipo kwa maslahi ya
mbowe na slaa pengine na watu wa kaskazini.
Kwa hiyo kuwazuia watu wenye
mawazo tofauti na wao na kuwaita wasaliti na wahaini ni sawa kuasisi na kuimiza
mpasuko ndani ya chama, maana kuna mambo kamati kuu inaweza kufanya na kuna
mengine haiwezi, hii haiwezi kufanya hili walilolifanya sasa hawawezi
kulifanya.
Nionavyo mimi na wanachama
ninaowaongoza hapa singida ni kwamba kamati kuu imekurupuka na kufanya maamuzi
yaliyotawaliwa na hofu, chuki na uroho wa madaraka dhidi ya zitto kabwe na
wenzake walioonyesha nia thabiti ya kukivusha chama kwenye harakati za
kuilikomboa Taifa.
MSIMAMO WA CHAMA
SINGIDA
(i)
Tunalaani, kuipinga na kuikemea kamati
kuu ya chama dhidi ya maamuzi yao haya ya kipuuzi yaliyojaa chuki, hofu na
wasiwasi mwingi kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani ya chama
(ii)
Tunamtaka mwenyekiti na katibu mkuu
waitishe mara moja mkutano wa baraza kuu la chama kutolea maamuzi suala hilo.
(iii)
Tunamtaka katibu mkuu awazuie wakurugenzi
na maafisa wake aliowatuma kusambaa mikoani kusambaza waraka wa siri
unaowachafua zitto na kitila na kwamba kufanya hivyo ni kujidharirisha wao
wenyewe.
(iv)
Tunampa onyo kali katibu mkuu Dkt. Slaa
kuwa asithubutu kukanyaga SINGIDA ikiwa bado hajayafanyia kazi maelekezo yetiu
hapo juu, kuzunguka kwake mikoani baada ya kumvua vyeo zitto ni kwenda
kuthibitisha kuwa amefanya makusudi mpango wake huo.
(v)
Tunapenda wanachadema na watanzania
watambue kuwa Hatuna Imani na Mwenyekiti wa Taifa wa chama, Katibu Mkuu wa
Chama, Kamati kuu kwa ujumla na tunamuagiza mbowe aivunje mara moja kisha nay
eye ajiudhuru.
MWISHO
Kutokutii maamizio yetu
haya ni kusababisha mgogoro usiokuwa na kikomo ndani ya chama hiki,
Singida tunasema kuwa ‘’
kamati kuu inaweza kumvua zitto kabwe uongozi, inaweza kumuondolea heshima yake
ndani ya jamii, inaweza pia kumsingizia kila aina ya uwongo itakavyo, lakini
kamwe kamati kuu haiwezi KUZUIA MPASUKO NDANI YA CHADEMA.’’
Kwa kuzingatia utangulizi
wangu hapo mwanzo, na kwa kuona ukweli kwamba chama chetu sasa kimevamiwa na
kuwa na vyama viwili ndani ya chama kimoja,
Nimeonelea ni vyema sasa
niilinde na kuithibitisha dhamira yangu ya demokrasia ya kweli, nimeona ni vema
nihakikishe demokrasia tunayoiimba tunaitenda kwa vitendo.
Kwa misingi hiyo sasa,
nimeamua kukaa pembeni ya udhalimu huu wa demokrasia unaoasisiwa na viongozi
wakuu wa chama wanaoogopa kivuli cha uchaguzi mkuu wa ndani ya chama,
Nimeona ni vema sasa
niuthibitishie umma wa Tanzania kuwa kwenye chadema unaruhusiwa kugombea vyeo na
nafasi zote isipokuwa uenyekiti wa Taifa ndio maana zitto tuliyemuunga mkono
leo hii anashambuliwa kwa dhamira yake safi ya kidemokrasia.
Nimechoka sasa, nimebadili
mawazo, sipo tayari tena kuwa msukule wa fikra mbele ya watu wanaopenda kuigiza
na kujifanya watetezi wa wanyonge kumbe ni wanafiki wa kutupwa.
Nimememuandikia barua
katibu wangu wa mkoa kumueleza maamuzi yangu ya kujiudhuru uenyekiti wa mkoa,
sihitaji tena kuwa mwenyekiti wa mkoa kwenye chama ambacho hakitendi
kinachoyasema, sihitaji tena kuwa mwenyekiti wa mkoa kwenye chama ambacho
dakika na saa yoyote unaweza ukageuzwa na ukaitwa msaliti na muhaini wa aina ya
kopekee.
Mimi kitundu, sihitaji
kuendelea kuwa dalali wa mafanikio ya kisiasa kwa ajili ya watu wa kaskazini
dhidi ya watanzania wenzangu.
Nimejiuzuru uenyekiti wa
mkoa wa SINGIDA kuanzia leo tarehe 3.11.2013 na kuahidi kuwa nitapambana mpaka
mwisho wa tone la damu ya uhai wangu kuhakikisha demokrasia ya ndani ya chama
hiki inaheshimiwa na kwamba watanzania hawadanganywi tena.
Nawashukuru sana.
Wilfred Noel Kitundu
Mwenyekiti Mkoa SINGIDA
Muasisi na mlezi wa
CHADEMA Singida 1992-2013
Mjumbe wa Baraza Kuu TAIFA
1992 – 2013
Mjumbe wa Mkutano Mkuu
Taifa 1992-2013
huo ni upepo mdogo sana!hauna impcts kabisa!alivuliwa uanachama hamad rashidi na kafulila!zaidi ndo wamejipotezea umaarufu tu!wakati hawa wachache wanaojiudhuru lakini tunasikia watu mashuhuri na wenye mvuto kwa jamii kuliko hata hao wanaojiudhuru,ila inakua wanajiunga na chama!tuone kama chama hakitapata mwenyekiti hapo singida!mimi mwenyewe nautaka sana huo uenyekiti nadhani ni wakati wangu kujisogeza hapo singida!
ReplyDelete