Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu –TAMISEMI, Jumanne Sagini (picahni)
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya wanafunzi
411,127 kati ya 427,609 sawa na asilimia 96.15 waliofaulu mtihani wa darasa la
saba 2013 wataanza kidato cha kwanza mwaka
ujao.
Kati yao wasichana ni 201,021 na wavulana 210,106 na huku
kiwango cha wanafunzi waliochaguliwa mwaka huu wakiwa wameongezeka kwa asilimia
31.37 ikilinganishwa na asilimia 64.78 waliochaguliwa awamu ya kwanza mwaka
huu.
Matokeo yanaonesha kuwa jumla ya wanafunzi 427,609 (wavulana
218,093 na wasichana 209.516) walifaulu kwa kupata alama A-C kati ya 844,938
waliofanya mtihani ikiwa ni sawa na asilimia 50.61 … takwimu zinaonesha
ongezeko la asilimia 19 la ufaulu ikilinganishwa na asilimia 30.6 mwaka jana.
Majina yao na shule wanazokwenda tafadhal ....
ReplyDeletetunayapata wapi majina ya walochaguliwaaaaa sasa
ReplyDeletemajina ya watoto mnayatoa lini ili tujue walikopangwa
ReplyDelete