Nafasi Ya Matangazo

December 24, 2013

Baada ya kushuhudia washindi kutoka mikoa mbalimbali nchini wakikabidhiwa zawadi zao zilizojumuisha Pikipiki maarufu kama Boda boda pamoja na fedha taslim kutoka katika Promosheni ya Timka na Boda Boda, Promosheni hiyo imeshuhudia kwa mara nyingine wakadhi wa jiji la  Dar es Salaam na sehemu zake nao wakikabidhiwa Bodaboda hizo hafla iliyofanyika katika makao makuu ya ofisi za kampuni ya Vodacom zilizoko Mlimani City.

Wakizungumza punde baada ya kukabidhiwa Pikipiki zao baadhi ya washindi wamesema wamefurahi kuibuka wahindi katika Promosheni hiyo huku wakitoa wito kwa Watanzania kuendelea kushiriki katika pomosheni hiyo ambayo imebakiza siku chache kumalizika.

“Nimefurahi ana na kufarijika kuwa mshindi wa Promosheni hiiya Timka na Boda Boda, Usafiri huu utanisaidia sana kutoka sehemu moja kwenda nyingine watu wengi wanajua namna usafiri kwa jiji a dar ulivyo mgumu lakini sasa nimepata suruhisho la tatizo hili nitakuwa nafika mahala pangu pa kazi kwa urahisi na kuondoka bila matatizo na kwa gharama nafuu, alisema Mzee Mustapha Bai, Moja ya washindi wa Pikipiki.

Kwa Upande wake Bwana, Steven Masawe ambaye ni Mwalimu wa VETA Amesema “Nimeshiriki promosheni hii kwa hari sana nikijua ipi siku nitashinda, na imekuwa kweli Pikipiki hii nitaipeleka kijijini kwetu migombani, Kibosho Moshi, ikawasaidie katika usafiri kwani kutoka kijijini kwetu hadi kufika mjini ni takribani kilomita 45 na usafiri ni wa tabu sana sasa kutokana na kuwa mteja wa Vodacom nimewatatulia tatizo la usafiri.

Miongoni mwa washindi ambao walikuwa kivutio kwa watu katika hafla hiyo ni ambaye ni mfanyakazi wa kazi za ndani Bi. Anastazia Nyangige alipowaambia washindi wenzake kuwa ametumia mshahara wake kushinda Bodaboda hiyo. “Mimi ni dada wa kazi za ndani sasa nitaendelea kufanya kazi zangu na kumtafuta kijana ambaye ataiendesha Boda boda hii na kuniletea fedha ili niweze kujiendeleza zaidi na ninaamini baada ya siku sitaweza tena kuendelea kuwa dada wa kazi na nitakuwa mjasiriamali, alisema Nyagige.

Akizungumzia juu ya promosheni hiyo Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amesema mpaka sasa kampuni yetu imekwishatoa bodaboda 230 huku  200 bado hazijatolewa mbali na hapo kuna kiasi cha shilingi milioni 142 tayari zimechukuliwa na milioni 178 zimebakia.

“Promosheni hii imekuwa yenye mafanikio makubwa sana kwani wateja wetu wameonesha mwitikio wa hali ya juu, promosheni hii inamlenga kila mtu kwani tatizo la usafiri ni letu sote na pia kilio cha watu kutokuwa na fedha za kukuza au kuongeza mitaji yao ya kibiashara ni kwa kila mtu. Kampuni yetu ni sikivu siku zote, tunawajali na kuwasikiliza wateja wetu na ndio maana tunawapatia kile wanachohitaji.” Aliongezea Nkurlu

Nkurlu aliongezea pia tunakabidhi bodaboda hizi kama sehemu ya sikukuu za Krisimas na mwaka mpya na huku tukiwaahidi kuja na huduma na ofa kemkem kwa ajili ya wateja wetu kwa mwaka ujao.

“Nawaasa washindi watakaopokea bodaboda hizi leo kuzitumia ipasavyo kwa usafiri au kuwekeza katika biashara na kuleta manufaa katika maisha yao. Pia ambao mpaka sasa hamjajiunga na promosheni hii, wakati ni huu kwani Januari mwakani zoezi hili litakamilika na nitasikitika kuona kwa nini hamshiriki kujishindia zawadi hizi.” Alimalizia Meneja huyo

Ili kujiunga na promosheni ya Timka na bodaboda wateja wote wa Vodacom wanatakiwa kuandika neno PROMO na kutuma kwenda nambari 15544.
Posted by MROKI On Tuesday, December 24, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo