Nafasi Ya Matangazo

November 18, 2013

WABUNGE wanaoiwakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki wamesema suluhisho la matatizo ya nchi za Maziwa Makuu yatapata ufumbuzi wa kudumu iwapo kutakuwa na utaratibu wa kukaa meza moja kwa pande zote husika na kufanya mazungumzo ya kuleta amani.

Hayo yalisemwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa wabunge hao, Adam Kimbisa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo pia alipongeza hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alioitoa Bungeni Dodoma Novemba 7 mwaka huu juu ya Jumuiya hiyo.

“Sisi tunaamini amani ni jambo la msingi katika Afrika Mashariki na hasa katika nchi zilizo katika Maziwa Makuu. Tunawapongeza wanajeshi wetu na wanajeshi Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa kazi nzuri walioifanya iliyowezesha mafanikio kupatikana” alisema.

Akielezea juu ya baadhi ya nchi wanachama wa EAC ambao ndio waanzilishi wa vurugu mbalimbali na migogoro Mwenyekiti huyo alisema kuwa Tanzania imekomaa kisiasa hivyo hawawezi kuwaondoa wale wanaoleta chokochoko kwa kuwa dawa ni kuzungumza na sio kuwatoa.

Mtangamano
Aidha Kimbisa amesema misingi ya Utengamano wa kiuchumi ikijengeka vizuri na kufanya kazi ipasavyo wananchi wote wa Afrika Mashariki watafaidika na hivyo suala la kuruka hatua yoyote ni jambo lisilokubalika.

“Tunaungana na kauli ya Rais kwamba Tanzania ni kati ya nchi zinazotaka ngazi zote za mchakato wa Mtangamano zitekelezwe moja baada ya nyingine bila kuruka hatua yoyote. Hatua ya kwanza ni Umoja wa Forodha inafuata soko la Pamoja kasha Umoja wa Fedha na hatimaye shirikisho la Kisiasa” alisema.

Alisema hadi sasa ni hatua mbili zilizotiwa saini na mchakato wa kuweka saini Umoja wa fedha unatarajiwa kutiwa saini baada ya kikao cha Juu cha Marais kinachotarajiwa kufanyika mjini Kampala Novemba 30 iwapo masuala yote muhimu ya mchakato huo yatakuwa yamekamilika.

 “Jambo la msingi ambalo hata Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya imesema wazi kwamba Jumuiya lazima iwe ni ya wananchi kwa manufaa ya wananchi na isiwe ya viongozi. Wananchi washirikishwe katika kila hatua na kila ngazi ili iweze kushiriki kikamilifu kwa ajili ya maslahi yao” alisema.


 Kuhusu VISA alisema kuwa wao wanaruhusu nchi nyingine kuendelea lakini Tanzania bado hawajafikia muafaka kwa kuwa wanaangalia maslahi ya nchi kwanza. Katika Hatua nyingine, Wabunge hao walimpongeza Rais Kikwete kupeleka kikosi cha Wanajeshi katika Brigedia Maalum iliyoundwa na Umoja wa Mataifa ili kuongeza nguvu ya kudhibiti waasi Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA),Adam Kimbisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wabunge hao wakitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa Bungeni hivi karibuni. Kushoto ni Katibu wa Wabunge hao, Shy-Rose Bhanji.
Kimbisa akizungumza na wanahabari Ukumbi wa Idara ya habari Maelezo.
wanahabari wakifuatilia hotuba hiyo..
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA),Adam Kimbisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana wakati wabunge hao wakitoa pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa Bungeni hivi karibuni. Kushoto ni Katibu wa Wabunge hao, Shy-Rose Bhanji. Kulia ni Mkurugezni Msaidizi wa MAELEZO, Zamaradi Kawawa.
Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Jumuia ya Afrika Mashariki (EALA),Adam Kimbisa akiteta jambo na Katibu wake, Shy-Rose Bhanji.
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shay-Rose Banji na Adam Kimbisa wakitoka katika Ukumbi wa MAELEZO Dar es Salaam leo baada ya kuzingumza na wana habari.
Posted by MROKI On Monday, November 18, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo