Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil
Colaso (wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na Meneja Uhusiano wa Timu ya
Manchester United, Bw. Michael Higham (wa kwanza kushoto). Kutoka kulia
ni Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Michezo, Bw. Leornad Thadeo, Rais
mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
na Mtangazaji
wa Clouds FM, Bw. Ephraim Kibonde muda mfupi baada ya uzinduzi wa promosheni ya
‘MIMI NI BINGWA’ iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es
salaam.
Baadhi
ya wadau mbalimbali wakifuatilia kwa umakini uzinduzi wa promosheni hiyo mpya
ya ‘MIMI NI BINGWA’ uliofanywa na Airtel Tanzania kwa ushirikiano na klabu ya
Manchester United.
Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde
ambaye alikuwa ni mshehereshaji wa uzinduzi wa promosheni ya ‘MIMI NI BINGWA’
akizungumzia promosheni mpya ya Airtel iliyozinduliwa jana katika hoteli ya
Hyatt Regency jijini Dar es salaam. Kutoka kulia ni Rais mpya wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, Mkurugenzi wa Maendeleo
ya Michezo,
Bw. Leornad Thadeo, Mkurugenzi wa Airtel Tanzania Sunil
Colaso pamoja na Meneja Uhusiano wa Timu ya Manchester United, Bw. Michael
Higham.
Mkurugenzi wa Airtel Tanzania, Bw. Sunil
Colaso akimkabidhi jezi ya Timu ya Manchester United, raisi mpya wa shirikisho
la mpira wa miguu Tanzania Bw. Jamal Malinz.
*********
KAMPUNI ya mawasiliano ya Airtel Tanzania imetangaza ushirikiano na klabu nguli
ya mpira wa miguu ya Manchester United ya nchini Uingereza utakaowezesha wateja
wa kampuni Airtel 10 kila mwezi kujishindia safari za kwenda kushuhudia mechi
za klabu hiyo moja kwa moja (live) katika uwanja wa Old Trafford.
‘Mimi
Ni Bingwa’ inalenga kuwazawadia wateja zawadi zenye thamani za zaidi ya
shilingi milioni 500.
Akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel
Tanzania, Sunil Colaso alisema ubia huo mpya unadhihirisha nia ya kampuni ya
kufurahisha na kutosheleza mahitaji ya wateja wake.
“Kampuni
ya Airtel Tanzania tunaingia ubia mpya na klabu ya Manchester United ambao
utawapa na nafasi wateja wetu wote na wapenzi wa Mpira fursa za kuangalia mechi
za timu ya Manchester United live katika uwanja wa Old Trafford.
“
Natoa wito kwa wateja wetu kuchangamkia fursa hii na kushiriki kikamilifu ili
kujishindia zawadi mbali mbali za kila siku, kila wiki na zawadi nono ya
shilingi milioni 50 itakayotolewa mwishoni mwa promosheni hii,” aliongeza.
Aidha
Colaso alisema kuwa kampuni yake imekuwa chachu ya maendeleo ya michezo mbali
mbali ikiwemo mpira wa miguu kupitia mkakati madhubutu wa kuendeleza mpira wa
miguu maarufu kama Airtel Rising Stars.
“Tunajivunia
kuwa mpango wetu wa Airtel Rising Stars imeanza kuvumbua vipaji nchini Tanzania
na barani Afrika kwa ujumla. Pia tunajivunia kuwa Tanzania imefanya vizuri
katika mashindano ya Airtel Rising Stars ya Afrika ya vijana chini ya miaka 17
yaliyofanyika nchini Nigeria miezi michache iliyopita,” aliongeza.
Naye,
Meneja Mahusiano wa Klabu ya Manchester United Michael Higham wakati wa hafla
hiyo alisema ubia wa klabu yake na kampuni ya Airtel ya Tanzania umelenga
kuongeza uwakilishi wa klabu hiyo nchini Tanzania.
“Tunafaraja
kupata ubia huu mpya na tuna matumaini kuwa hii itakuwa fursa nzuri ya
kuwapatia na kujionea mechi kali moja kwa moja. Bila shaka, tunategemea kuwa
ushirikiano huu utatusaidia kuongeza mashabiki hapa Tanzania,” alisema Higham.
Aidha,
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana
Utamaduni na Michezo, Leonard Tadeo wakati wa hafla hiyo aliipongeza kampuni ya
Airtel kwa kuendelea kusaidia maendeleo ya sekta ya michezo nchini.
“Nachukua
nafasi hii kuishukuru kampuni ya Airtel Tanzania kwa jitihada zake za kuendelea
kusaidia maendeleo ya michezo nchini hususani Airtel Rising Stars ambayo
imeibua vipaji kama Serengeti Boys na Timu ya Tanzanite kwa wasichana ambao
wamekuwa wakiiwakilisha nchi vizuri katika michezo ya kimataifa,” alisema
Tadeo.
Wakati
huo huo, Rais wa Shiriko la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi wakati
wa tukio hilo naye aliishukuru Airtel kwa uhusiano wake wa muda mrefu na
shirikisho na kuyaasa makampuni mengine kusaidia maendeleo ya michezo nchini.
“Kampuni
ya Airtel Tanzania imekuwa ni chombo muhimu katika maendeleo ya michezo ikiwa
ni pamoja na mpira wa miguu kupitia mpango wake wa Airtel Rising Stars ambao
umetuletea heshima kubwa kimataifa miezi michache iliyopita.
“TFF
itaendelea kufanyakazi kwa ukaribu na wadau mbali mbali ili kuhakikisha
tunaupeleka mchezo wa mpira wa miguu nchini katika ngazi ya juu zaidi,”
alisema.
Zawadi
za thamani ya zaidi ya milioni 500 zitashindaniwa katika promosheni ya ‘Mimi
ni Bingwa’ na Airtel Tanzania.
Washindi
katika promosheni hiyo watajishindia jezi halisi za timu ya Manchester United,
fedha taslim kila siku na kila wiki na zawadi kubwa ya shilingi milioni 50
mwishoni mwa promosheni.
Ili
kushiriki kwenye promosheni ya Airtel MIMI NI BINGWA mteja anatakiwa
kutuma ujumbe mfupi (SMS) ukiwa na neno “BINGWA” kwenda namba 15656 .
0 comments:
Post a Comment