Mkuu
wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,Ofisi ya Rais Sekretariati ya Ajira
katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham (kushoto) akizungumza na vyombo vya
habari nchini juu ya Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma,
kwenye mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO)Jijini
Dar es Salaam,kulia ni Katibu Msaidizi Idara ya Ajira kutoka Ofisi hiyo Bw.
Malimi Muya.
**********
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo kilichoundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29 (1).
Jukumu la msingi la Sekretarieti ya Ajira ni kuendesha mchakato wa ajira
katika Utumishi wa Umma. Hapa ina
maana kuwa jukumu la kuajiri,
kuthibitisha watumishi kazini pamoja na masuala ya nidhamu ya Watumishi
yanabaki kwa Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi katika Utumishi wa Umma mitarafu ya Kifungu cha 6(1) (b) cha Sheria
ya Utumishi wa Umma no 8 ya mwaka 2002.
Ambapo katika kuendesha mchakato
huo, Sekretarieti ya Ajira inapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni, na Taratibu zilizopo
ili kuhakikisha Utumishi wa Umma unapata Watumishi weledi na wenye maadili mema.
Hadi sasa jumla ya waombaji 4891 tumeshaendesha mchakato wao wa ajira na kuwapangia
vituo vya kazi.
Hata hivyo, Sekretarieti ya Ajira kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais
Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilipeleka Mswada Bungeni unaopendekeza kukasimu
madaraka ya kuendesha mchakato wa Ajira ili baadhi ya Waajiri wakasimiwe
madaraka hayo ili kurahisisha utendaji kazi katika kushughulikia mchakato wa ajira kwa baadhi ya kada.
Huku Sekretarieti ya Ajira ikiendelea kuhakikisha kuwa jukumu hilo
linaendelea kutekelezwa kwa ufanisi. Tunapoongelea suala la ufanisi hapa
Kitengo cha Udhibiti na Ubora kinasimamia suala zima la uhakiki wa taarifa za
mhusika, uhakiki wav yeti na uadilifu wake kwa ujumla.
Ambapo hadi sasa
tumeshakamata jumla ya vyeti vya
kughushi 677 ambavyo wahusika wanadai wamevipata kutoka RITA, VETA na NECTA.
Nafasi wazi za kazi zitakazokuwa
zikitangazwa na mchakato wake kuweza kukasimiwa ni pamoja na Kada ya Wasaidizi
wa ofisi, Wahudumu wa afya, Madereva, Maafisa Watendaji wa Kata, Mtaa, Kijiji,
Wapishi, Walinzi, Madobi, Wasaidizi watunza kumbukumbu pamoja na Makatibu
Muhtasi (walio chini ya cheo cha mwandishi mwendesha ofisi) au Kada zingine ambazo Katibu wa Sekretarieti
ataona inafaa kukasimu.
Aidha, nitoe ushauri kwa wanafunzi walioko shuleni na wanaotarajia
kuingia vyuoni kuchukua masomo ama kozi za fani ya Afya, Elimu, Mifugo na
Kilimo maana ni maeneo ambayo bado yana fursa nyingi za ajira Serikalini na
wahitimu wake pindi wamalizapo wanapangiwa vituo vya kazi moja kwa moja bila ya
kupitia mchakato wetu wa ajira kutokana na uhaba wa Wataalam wa fani hizo
katika soko la ajira hivi sasa.
Sekretarieti ya Ajira katika kuhakikisha
wananchi wanapata taarifa kwa haraka
zaidi zinazohusu mchakato wa ajira
katika Utumishi wa Umma na ili kuweza
kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia ya habari na mawasiliano nchini na
duniani kwa ujumla, iliamua kuanzisha tovuti yake (www.ajira.go.tz) ambayo imerahisisha kwa kiasi kikubwa utoaji na upokeaji wa
taarifa mbalimbali hususani za matangazo ya fursa za ajira taarifa
nyingine zinazohusu masuala ya ajira Serikalini na matangazo mengine yanayohusu
shughuli za Sekretarieti ya Ajira. Tangu kuzinduliwa mwezi Aprili, 2013 imeweza
kutembelewa na wadau zaidi ya 2,900,000.
Pamoja na tovuti Sekretarieti ya Ajira
imeanzisha KANZIDATA (DATABASE) za aina tatu (3) ambazo ni Kanzidata ya
Wahitimu wa Vyuo, Kanzidata ya waliofaulu usaili na Kanzidata ya waliopangiwa
vituo vya kazi.
Jambo lingine ambalo ningependa mkalifahamu ni
kuwa, Sekretarieti ya Ajira iko katika hatua za awali za mchakato wa kuwawezesha
waombaji wa fursa za ajira kuwasilisha maombi ya kazi kwa mfumo wa kielektroniki
(e-application) kwa nafasi wazi zitakazokuwa zikitangazwa katika Utumishi wa
Umma ili kurahisisha kupunguza mlolongo wa uendeshaji mchakato wa ajira ulivyo
hivi sasa.
Mwisho nimalizie kwa kuwataka waombaji wa fursa za ajira kutokuchagua
maeneo ya kufanyia kazi, hususani wale wanaopangiwa vituo vya kazi na
Sekretarieti ya ajira na hawaendi kuripoti bila ya kutoa sababu za msingi maana
Sekretarieti ya Ajira inaona hili ni kosa na inaandaa utaratibu wa kutowaruhusu
kufanya usaili mwingine waombaji kama hao.
Imetolewa na Riziki V. Abraham, Msemaji na Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa
Umma +255-687624975
0 comments:
Post a Comment