Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza
Uhandisi wa Kompyuta wa chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Wendy Habakuki Lwendo
amefariki dunia katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni
akiogelea na wenzake watatu jana jioni.
Akizungumza na Father Kidevu Blog, kaka
wa Marehemu, Sammy Lwendo amesema mdogo wao alipatwa na maswahibu hayo akiwa na
rafiki zake hao watatu wakiogelea baharini na wakati wanaogelea walikuwa katika
eneo la kina kifupi cha maji yaliyokupwa na mara maji hayo yaka jaa na
walipokuwa wakijaribu kutoka ndipo Wendy akazidiwa na maji.
Lwendo amesema kuwa wenzake
walifanikiwa kumtoa majini lakini hali yake tayari ilikuwa mbaya na kwakuwa
hawakuwa na ujuzi wa kutosha wa kutoa huduma ya kwanza kwa mtu aliyezama majini
walihangaika kwa zaidi ya dakika 40 kumsaidia ndipo wakapata msaada wa Polisi kumkimbiza kituo cha afya Kibaoni huko
Kigamboni lakini jitihada za kuokoa maisha yake ziligonga mwamba.
Aidha alisema kuwa mwili wa
Marehemu ulihamishiwa katika Hospitali ya Wilaya Vijibweni na sasa ndugu
wamefika na kuhamishia mwili huo Hospitali ya jeshi Lugalo.
Msiba kwa sasa upo Kinondoni
nyuma ya Vijana, huku wakisubiriwa wazazi wa marehemu pamoja na ndugu wengine
ili kujua taratibu kamili za maziko.
Wazazi wa Wendy, Mchungaji Habakuki Lwendo ni mwalimu wa Chuo cha Uchungaji Makumira mkoani Arusha.
0 comments:
Post a Comment