Meneja wa bia ya Serengeti Allan Chonjo(katikati) akiongea na wana habari wakati wa kumtangaza mshindi wa droo ya tatu ya Winda na Ushinde ambaye ni Bi Blanca Mariki, katika ofisi za Kampuni ya Bia ya Serengeti jana jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na wadau wengine wa droo hiyo Meneja mauzo wa Push Mobile Rugambo Rodney(kulia) na Afisa mwandamizi kutoka PWC Daniel Nnko (kushoto).
********
Kampuni ya bia ya Serengeti imetangaza mshindi wa droo ya mwisho ya
promosheni ya Winda na Ushinde ambae amejinyakulia kitita cha milioni moja
baada ya kuchezesha droo yake ya tatu na ya mwisho. Droo hiyo ilichezeshwa
katika ofisi za kiwanda hicho jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa na mhakiki
kutoka katika bodi yamichezo ya Bahati
Nasibu.
Baada ya kupokea simu Blanca Mordest Mariki(30) anayefanya biashara
ndogo ndogo kutoka Morogoro alionesha furaha yake na kubaki bumbuwazi kwa
furaha. “Nimefurahi sana kuwa mshindi wa promosheni hii ya Winda na Ushinde
kutoka katika kampuni ya Bia ya Serengeti.
Na najivunia kuitumia bia ya
serengeti kwani ndio bia niipendayo na nawapongeza sana kampuni ya Serengeti
kwa kuanzisha mashindayo haya” Pamoja na ushindi huu mkubwa nimeshajishindia
bia za bure za Serengeti mara mbili, pamoja na hela taslimu shilingi 10,000
mara nne ambazo huwa natumiwa kupitia njia ya simu”. Alisema mshindi huyo.
Akiongelea promosheni hii meneja wa kinywaji cha bia ya Serengeti Allan
Chonjo alisema “promosheni hii ni ya kipekee na mpaka sasa watanzania wengi wameshajishindia
bia za bure na pesa taslimu ambazo ni shilingi 10,000 na100,000/= na pia washindi wetu wakubwa wa droo ya
kwanza na ya pili walijishindia milioni moja kila mmoja.
Mshindi wa droo ya
kwanza alitoka Kilimanjaro na mshindi wa pili alitoka Dar es Salaam na wote waliipongeza
sana kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuwasaidia wateja kwani wameinua uchumi
wao kupitia ushindi wao wa promosheni hii”.
“Lengo
la kampuni yetu ni kuendeleza umoja na mshikamano na wateja wetu kwa kuutambua na kuuthamini mchango
wao kwani wao ni muhimili mkubwa katika kukuza na kuendeleza bia yetu ya
Serengeti.
Promosheni hii inaendelea mpaka mwisho wa mwezi Julai na kumalizika
kwa promosheni ya Winda na Ushinde ni mwanzo wa mengine mengi yanayotolewa na
kampuni ya bia ya Serengeti kwa ajili ya wateja wetu”. Aliongeza meneja huyo.
Tafadhari kunywa kistaarabu na ni maalum kwa 18+
0 comments:
Post a Comment