Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali mtoto Kelvin Albert (3) aliyelazwa katika Hospitali ya
Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu
uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt.
Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha. Kushoto ni Mama
wa mtoto huyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali mtoto Deric Siprian Kessy (8) aliyelazwa katika
Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa
Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt.
Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha. Kushoto kwa
Makamu ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo na (kulia) kwa Makamu
wa Ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Dkt. Alex Malasusa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali mtoto Gabriel Godfrey (9) aliyelazwa katika Hospitali ya
Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu
uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt.
Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali Restuta Alex (50) aliyelazwa katika Hospitali ya Mount
Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea
katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la Katoliki Mt. Joseph
Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali mmoja kati ya wagonjwa waliokuwa mahututi, aliyelazwa
katika Hospitali ya Mount Meru, baada ya kujeruhiwa katika tukio la
mlipuko wa Bomu uliotokea katika hafla ya uzinduzi wa Kanisa jipya la
Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti jana mchana, jijini Arusha.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimfariji Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la
Olasiti, Josephat Lebulu, wakati alipowasili nyumbani kwa askofu huyo
jijini Arusha jana kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu
lililotokea jana mchana, jijini Arusha kwenye hafla ya uzinduzi wa
Kanisa hilo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Balozi wa Vatcan na mwakilishi wa papa Francis, Askofu
Francisco Montecillo, walipokutana nyumbani kwa Askofu Mkuu wa kanisa
Katoliki Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti, Josephat Lebulu, alipofika
kumfariji kutokana na tukio la mripuko wa bomu lililotokea jana mchana,
jijini Arusha.
Ninaungana na Watanzaniawenzangu kuwatakia faraja ya Mungu ndugu zetu waliofiwa na ndugu zao ktk mlipuko wa Arusha. Pia ninawaombea majeruhi Mungu awape uponyaji wa haraka.
ReplyDeleteNinaomba kwa ajili ya amni ya nchi yetu na pia Mungu atusaidie kuwapata haraka wahusika wa mlipuko na kujua nia na mipango yao juu ya kuhatarisha amni ya nchi yetu.
MUNGU AIBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.
Mchg. Fadhili J. Lyamuya