Afisa
Mpango Mwandamizi Bw. Peter Amos akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dar es salaam kuhusu wiki ya nenda kwa usalama barabarani itakayofanyika tarehe
11 Mei, 2013 katika shule ya Sekondari Turiani iliyopo Kinondoni jijini Dar es
salaam.
*******
Na Elphace Marwa - MAELEZO.
SHIRIKA
lisilo la kiserikali linalojishughulisha na usalama barabarani AMEND Organisation kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi kitengo cha Usalama barabarani wameandaaa matembezi mafupi ya kuukumbusha umma kuhusu hatari za
barabarani wanazokabiliana nazo watembea kwa miguu.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Afisa Mpango Mwandamizi wa AMEND
Bw. Peter Amos amesema kuwa kwa kipindi
cha mwaka 2012 takribani watu
wasiopungua elfu nne walipoteza maisha kwa ajali za barabarani ambapo asilimia
30 kati yao ni watembea kwa miguu.
Bw.Amos
amesema kuwa matembezi hayo yatafanyika jumamosi tarehe 11 mwezi mei kuanzia
saa tatu asubuhi katika shule ya sekondari ya Turiani wilaya ya Kinondoni.
Aidha
Amos amesema matembezi hayo yanalenga kuhamasisha watu kuchukua tahadhari
wanapokuwa barabarani ili kulinda usalama wao na watembea kwa miguu.
“Tumejitahidi kutoa elimu ya usalama barabarani katika
shule za msingi na sekondari na kutoa elimu kwa madereva pikipiki kwa lengo la
kupunguza vifo na majeruhi wa ajali za barabarani.”
Bw.Amos
ameeleza kuwa jumla ya madereva 300 wa bodaboda wamepatiwa mafunzo na wameweza kufaulu
vipimo vya udereva na kupatiwa leseni .
Kwa
upande wake Mrakibu wa Jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Bonaventura
Nsokolo kutoka trafiki Makao makuu
ametoa wito kwa waandishi wa habari kuelimisha jamii juu ya matumizi
bora ya barabara kwani ajali za barabarani zimekuwa zikigharimu maisha ya
watanzania wengi wasio na hatia.
Wakati
huohuo Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika
lisilo la kiserikali la Helmet Vaccine Initiative Tanzania Bw. Alpherio Nchimbi
amesema taasisi yake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine wana
lengo la kupunguza kwa asilimia 50 vifo vinavyotokana na ajali za barabarani kufikia mwaka 2020.
Wageni
rasmi akiwemo Kamanda Mpinga wa Kikosi
cha Usalama barabarani wanatarajiwa kuzungumza
na wananchi siku hiyo ili kuwahamasisha kujilinda na ajali za barabarani na
kupunguza vifo vitokanavyo na ajali za barabarani.
0 comments:
Post a Comment