Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi.
Regina Kikuli akionesha ufunguo wa gari wa moja ya
magari saba yaliyotolewa leo (jana) ,ambapo ni msaada kutoka
WHO na vifaa vingine vyenye thamani ya sh. bilioni 2.4 katika hafla
iliyofanyika jijini Dar es Salaam. katika hafla iliyofanyika jijini
Dar es Salaam. Katika msaada huo magari mengine 22 yatatolewa baade.
**** *****
NA FRANK JOHN – MAELEZO
SHIRIKA la Afya Duniani ( WHO)
limekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali wenye thamani sh. bilioni 2.4
kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kusadia katika kupunguza
vifo vya watoto wachanga walio chini ya miaka mitano na kuiwezesha Mamlaka ya
Chakula na Dawa (TFDA) katika utendaji wake.
Msaada huo umetolewa leo (jana) na Mwakilishi Mkazi wa
WHO Dk. Rufaro Chatora , ambapo alimkabidhi Naibu Katibu Mkuu wa wizara
hiyo, Bi. Regina Kikuli katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi msaada huo, Dk.
Chatora amesema shirika hilo linathamini juhudi za serikali katika
kupunguza vifo vya watoto ndio maana linaipongeza kwa kutimiza malengo ya
milinea ambapo watoto wote wamefaidika na malengo hayo.
Alivitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni
majokofu 128,komputa nne magari saba ya aina mbalimbali mashine za
kutolea kopi,vifaa vya kufuatilia ubaridi ndani ya majokofu yatakayotumika
kutunza dawa kwa ajili ya chanjo za watoto walio chini ya miaka mitano,
vifaa vingine kwa ajili ya kusaidia TFDA.
Akizungumzia kuhusu msaada huo, Bi Kikuli
alibainisha kuwa umekuja kwa wakati muafaka ambapo serikali imekuwa
ikishirikiana vyema na washirika wa maendeleo katika kutimiza malengo ya
milenia hasa lengo la nne na tano ambayo yanalenga kuboresha sekta ya
Afya kwa kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano kwa
kuwapatia chanjo stahiki kwa wakati kwa kuwa chanjo ni haki ya kila
mtoto.
Aliongeza kuwa serikali ya Tanzainia imefanikiwa
kwa kiasi kikubwa kutekeleza malengo ya milenia hasa lengo namba nne
ambalo ni kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano,
ambapo vifo hivyo vimepungua kutoka kutoka 147 kwa vizazi hai 1000 hadi 81
mwaka 1999 na vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja kutoka 99 kwa vizazi
hai 1000 hadi 51 katika kipindi cha mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment