Washindi
wa kipindi cha kwanza cha Guinness Football Challenge kilichooneshwa jana
katika Televisheni za ITV na Clouds TV Mwalimu Akida Hamad(kushoto) na Daniel
Msekwa(kulia) katika picha ya pamoja na waenesha kipindi Flora Tumsiime na
Larry Asego jana baada ya kipindi.
Timu zilizoshiriki kipindi cha kwanza cha
Guinness Football Challenge kutoka kushoto wenye nyekundu ni timu kutoka Kenya
Stephen Githinji na Michael Kirwa, wenye bluu ni Mwalimu Akida na Daniel Msekwa
timu kutoka Tanzania, wenye rangi ya kijani ni timu kutoka Uganda Kennedy
Andindu na Oscar Boban na mwsho timu nyeusi pia ni kutoka Kenya Oscar Litonde
na Daniel Muthendu.
***** ****
Jana usiku kupitia
televisheni za ITV na Clouds TV za
jijini Dar Es Salaam,kwa staili ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™, Daniel Msekwa na
Mwalimu Akida Hamad kutoka Tanzania walioonesha kwamba hakuna kisichoshindikana na hakuna kufa moyo
kabisa katika mchezo huu ambao sasa hivi unatazamwa na wengi barani Afrika.
Wawili hao waliishia kwenye
sare kwa raundi mbili na kuthubutu kuingia kwenye nusu fainali ambapo wana nafasi ya kupandisha kitita chao
hadi dola za kimarekani 5,500 (USD 5500)
kwenye ukuta wa pesa wa Guinness.
Daniel na Mwalimu walionesha
umuhimu wa kutokata tamaa na sasa wameingia kwa kishindo kikubwa kuwakilisha
Tanzania kupambana na nchi zingine za Afrika.
Kwenye raundi hii ya kucheza na nchi zingine zilizokuwa kwenye jumuiya
ya Afrika mashariki, ikumbukwe kuwa kuna
dola za kimarekani 250,000 ($250,000) za kushindaniwa .
Wiki ijayo tutaweza kuona timu
zingine nne kutoka hapa hapa Afrika mashariki zikichuana vikali na kuonesha umahiri
wao, Je wataweza kuingia na kuwakilisha nchi zao kupambana na nchi zingine za
Afrika? Je timu nyingine kutoka Tanzania
itaweza kuwapiga chini wakenya na waganda ili tuwe na timu mbili kwenye raundi
ya ‘Pan Africa ’?
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga kinachotayarishwa na
kampuni ya kimataifa ya Endemol. Kipindi hiki kuanzia jana kitakua kinarushwa
kila Jumatano katika televisheni za ITV na clouds TV, kwa ITV itakua ni saa
tatu na dakika kumi na tano(3:15) usiku
na saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku Clouds TV.
Usisahau kuwa na chupa ya
bia uipendayo ya Guinness wakati ukitazama
kipindi hiki.
*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi na nane. Tafadhali Kunywa kistarabu.
0 comments:
Post a Comment