Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania inaendelea kesho
(Machi 27 mwaka huu) kwa mechi mbili ambapo bingwa mtetezi Simba atakuwa
mgeni ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Uwanja
huo wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 3,000 unatarajiwa kushuhudia
mechi yenyen ushindi kutokana na uwezo wa wachezaji wa pande zote mbili.
Mechi
nyingine itapigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es
Salaam kati ya wenyeji Azam na Tanzania Prisons kutoka Mbeya.
TENGA AHIMIZA VIGEZO U15 FIFA COPA COCA-COLA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga
amewataka viongozi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa kuhakikisha
wanaingiza wachezaji wenye umri sahihi katika michuano ya U15 FIFA Copa
Coca-Cola 2013.
Ametoa
mwito huo leo (Machi 26 mwaka huu) wakati akifungua semina elekezi ya
michuano ya Copa Coca-Cola ambayo kuanzia mwaka huu itakuwa
ikishirikisha watoto wenye umri chini ya miaka 15.
Rais
Tenga amesema hakuna jambo la kipuuzi kama kuchomekea wachezaji ambao
wamezidi umri unaotakiwa kwa vile lengo la michuano ya aina hiyo ni
kubaini vipaji na kuwafanya watoto wapende kucheza mpira wa miguu.
“Kwanza
nawashukuru kwa kutenga muda wenu na kuhudhuria semina. Lakini ni
vizuri pia mkahakikisha mnakuwepo kwenye mashindano ili kutekeleza haya
ambayo tutakubaliana katika semina hii. Mkileta mtu mwingine anaweza
kutuanzishia mambo mengine badala ya yale tutakayokubaliana,” amesema
Tenga.
Pia
ameishukuru kampuni ya Coca-Cola ambaye imekuwa ikidhamini michuano
hiyo tangu mwaka 2007 ambapo semina hiyo elekezi inayoshirikisha
makatibu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na waratibu wa mikoa wa
michezo ya UMISSETA ni ya saba mfululizo.
Ratiba
ya michuano hiyo kuanzia mwaka huu imebadilika ambapo sasa itaanzia
ngazi ya wilaya Aprili wakati fainali katika ngazi ya Taifa itachezwa
Septemba.
0 comments:
Post a Comment