Nafasi Ya Matangazo

March 24, 2013

 Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars),Thomas Ulimwengu akiwatoka Golikipa na Beki wa Timu ya Taifa ya Morocco wakati wa Mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu kucheza Kombe ya Dunia Mwaka 2014 kule nchini Brazil,uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imeshinda Bao 3 - 1,mabao yaliyotiwa kimiani na Mshambuliaji Machachari,Mbwana Samatha na Thomas Ulimwengu.
 Ubao wa Matokeo unavyosomeka mara baada ya kumalizika kwa mechi kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Timu ya Taifa ya Morocco uliochezwa jioni hii kwenye uwanja wa Taifa wa Jijini Dar es Salaam. 
*********
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wanaosakata soka la Kulipwa nchini Kongo DRC, katika timu ya TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu leo wamewathibitishia kile ambacho waliwaahidi watanzania siku kadhaa zilizopita wakati walipowasili nchini kujiunga na kambi ya timu ya taifa.

Samatta na Ulimwengu waliwaahidi watanzania ushindi dhidi ya timu ya Morocco katika mchezo wa kundi C kuwabnia kufuzu fainali za kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.

Alikuwa ni Thomas Ulimwengu aliyewanyanyua mashabiki na wapenzi wa Soka Tanzania baada ya kuipatia Taifa Stars bao la kuongoza katika dakika ya 46 ya kipindi cha pili.

Dakika ishiri baadae Mbwana Samatta alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Thomas Ulimwengu ambaye nae alipokea pasi toka kwa Athuman Idd ‘Chuji’ bao lililofungwa dakika ya 66.

Alikuwa ni Mbwana Samatta tena aliyewanyanyua watanzania katika viti baada ya kupachika msumari wa mwisho mnamo dakika ya 86 akimalizia pasi ya Ulimwengu.

Morocco walipata goli lao la kufutia machozi katika dakika ya 90 +4 kupitia kwa Yousef Elarabi.

Kwa matokeo hayo, Stars inaendelea kushika nafasi ya pili katika Kundi C kwa pointi zake sita, nyuma ya Ivory Coast inayoongoza kwa pointi zake saba, baada ya jana kushinda 3-0 dhidi ya Gambia.

Stars sasa inakabiliwa na kibarua kigumu kwa mechi mbili za ugenini dhidi ya Morocco na Gambia huku Ivory Coast wakisubiriwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Viosi vya leo ni
Taifa Stars:- Juma Kaseja (Nahodha), Erasto Nyoni, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, Aggrey Morris, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Mrisho Ngassa/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk 63, Frank Domayo, Mbwana Samatta/Jahn Bocco dk 91, Mwinyi Kazimoto/Thomas Ulimwengu dk46 na Amri Kiemba.

Morocco:- Nadir Lamyaghri, Younes Belakhadr, Abdelilah Hafidi/Nuredenne Amrabat, Zakarya Bergdich, Abderrahim Achchakir, Younes Hammal, Abdelaziz Barrada, Issam Eladoua, Kamal Chafni, Chahir Belghazouani/Youssef El Arabi na Hamza Abourazouk.  
 
Posted by MROKI On Sunday, March 24, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo