Wasanii wa Tanzania, Joseph Haule ‘Prof. J’ pamoja na Nice
Mkenda ‘Mr Nice ni miongoni mwa wasanii kadha wa Afrika Mashariki ambao
watapamba tamasha la badilisha live nchini Uganda.
Tamasha hilo kubwa la burudani linaloratibiwa na
Mwanamuziki wa Bongo Fleva wa nchini humo Dk. Jose Chameleone linataraji kufanyika
Aprili 26, mwaka huu katika viwanja vya Rugby vya Kyadondo.
Akizungumzia
Tamasha hilo Chameleone katika moja ya kurasa zake za Facebook na Twitter,
amesema mambo yanaebnda poa na Wasanii kibao wamethibitisha kushiriki tamasha
hilo.
Mbali
na Prof. J na Mr Nice kutoka Tanzania, wengine ni Redsan kutoka Kenya, Massamba wa nchini Rwanda.
0 comments:
Post a Comment