Mkulima wa nchini kutoka Worcester mjini wa Western
Cape nchini Afrika
Kusini Johan du Plessis amevinja rekodi
kwa boga lake kuwa na uzito wa kilo 417.5.
Plessis ambaye ni mkulima anae karibia kustaafu
shughuli za kilimo kutokana na umri wake kumtupa mkono, amevunja rekodi ya nchi
hiyo kwa kuzalisha Boga kubwa kuliko yote kuwahi kutokea nchini humo.
Mazao
ya mboga mboga ambayo huwa na uzito mkubwa hupata tuzo wakati wa maonesho
maalum ya Diemersdal Durbanville Wine Estate’s wakati wa mashindano ya maboga
yaliyofanyika hivi karibuni.
Mtoto
wa Plessis aitwae Henri ndiye alikuwa akishikilia rekodi ya mwaka uliopita kwa Boga
lililokuwa na uzito wa kilo 390. Henri mwaka huu ameshika nafasi ya tatu kwa
Boga lenye uzito wa kilo 376.5
Alipoulizwa ni namna gani mkulima anaweza
kuzalisha Maboga ya uzito huo, Plessis alisema hakuna la zaidi ya kuliangalia
kwa umakini, ikiwa ni pamoja kuyakinga na jua, kuyapa nafasi ya kutosha majani
na matunda pamoja na kuhakikisha udongo upo katika hali nzuri.
0 comments:
Post a Comment