MCHEKESHAJI
maarufu na mwimbaji wa muziki wa Injili nchini, Emmanuel Mgaya, Masanja
Mkandamizaji, amesema kuwa amejipanga imara kuhakikisha kuwa anafanya
vitu vya aina yake katika onyesho la Tumaini Jipya, linalotarajiwa
kufanyika mkoani Morogoro Machi 31, katika Uwanja wa Jamhuri na
kushirikisha pia waimbaji mbalimbali nchini.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Masanja alisema kuwa amejiandaa vyema kutangaza
neon la Mungu kwa kupitia kipaji chake cha uimbaji wa muziki wa Injili,
akiamini kuwa afya yake itakuwa njema na kuimba pamoja na wadau wao
katika onyesho hilo la Tumaini Jipya.
Alisema
ingawa anatamba sana katika ulingo wa uchekeshaji kwa kuwa na aina ya
uzungumzaji na kufurahisha watu wengi, lakini makali yake hayaelezeki
katika uimbaji wa muziki wa injili. “Nipo
sawa kiafya na naamini Mungu atanibariki kila zuri kwa ajili ya kuimba
pamoja kwenye tamasha hilo la Tumaini Jipya nikiwa na waimbaji wengine
wenye makali ya aina yake.
“Itakuwa
ni siku nzuri kwa siku ya Jumapili ya Machi 31 katika uwanja huo wa
Jamhuri, hivyo naamini watu watakuja kwa wingi kulishuhudia neno
likipenya masikioni mwao,” alisema Masanja Mkandamizaji.
Mbali
na Masanja, wengine watakaofanya onyesho hilo ni pamoja na Martha
Mwaipaja, Stara Thomas, Bahati Bukuku, Sifa John, Joseph Nyuki pamoja na
vikundi mbalimbali vya kwaya vikitajwa kuwapo kwenye tamasha hilo la
Tumaini Jipya litakaloanzia mkoani Morogoro.
0 comments:
Post a Comment