Jarida
la katuni linaloandaliwa na mchoraji katuni, Nathan Mpangala, limeanza
kurushwa leo, Alhamisi, likiwa na sura mpya kwa kusheheni katuni kibao
ili kukidhi haja ya wapenzi wa katuni wa ndani na nje ya nchi.
Jarida hilo ambalo litakuwa likipatikanakwenye link; www.nathanmpangala.blogspot.com,
linatambulikwa kwa jina la ‘Jarida la Katuni la Nathan’ au kwa
kidhungu; ‘Nathan Cartoons Magazine’ linalenga kuongeza wigo wa matumizi
ya katuni nchini kwani kwa miaka mingi, katuni zimekuwa zikitumika
zaidi kwenye zaidi kuliko njia zingine.
Jarida hilo litakuwa likipambwa
na katuni za kisiasa, uchumi, michezo na karakta maarufu zilizokuwa
zikitoka magazetini siku za nyuma kama; Kijasti, Mzungu Mtaani, Daladala
Laivu nk. Pia litakuwa na katuni mahsusi kwa ajili ya anga za
kimataifa.
Mbali na katuni pia litakuwa na
habari mbalimbali za mashindano ya katuni yanayoendelea ulimwenguni ili
kuwawezesha wachoraji wa Kitanzania kushiriki.
0 comments:
Post a Comment