Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso Akibandika moja ya kipeperushi cha Airtel
yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wake na kutoa elimu ya
huduma zao ikiwemo Airtel
Yatosha inayompa mteja, Simkadi moja, taifa moja na bei moja.
Mkurugenzi
wa kitengo cha Mauzo Mustapha Kapasi( kushoto) pamoja na Gaspa Mroso waakiongea na wateja wakati wafanyakazi wa Airtel
walipotembea wateja wake na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo Airtel
Yatosha
Meneja
wa kitengo cha network, Emmanuel Luanda akisajili wateja kwenye huduma ya Airtel Yatosha wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wake na kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo Airtel Yatosha mwishoni mwa wiki hii.
Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso akiongea na meneja wa Uhusiano wa Airtel
Jackson Mmbando wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembea wateja wake na
kutoa elimu ya huduma zao ikiwemo Airtel Yatosha inayompa mteja, Simkadi
moja, taifa moja na bei moja.
Afisa Mauzo wa Airtel bi Theresia Kimaro
Akiongea na wateja juu ya huduma ya Airtel yatosha wakati Airtel walioko
Magomeni na kutoa elimu juu ya huduma mbalimbali ikiwemo ya Airtle yatosha.
****** ********
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea
kusambaza huduma ya Airtel yatosha katika mikoa mbalimbali nchini baada ya
kuzindua huduma mpya ya punguzo la upigaji simu maarufu kama Airtel YATOSHA
katikamikoa ya kanda ya ziwa.
Airtel sasa imeanza kuitambulisha huduma
hiyo kwa wadau na wateja wake katika mikoa mbalimbali nchini ili waweze
kunufaika nayoHuduma ya Airtel Yatosha inamuwezesha mtumiaji wa mtandao
wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao
yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha
kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine.
Akionge wakati wa utambulisho wa huduma ya
Airtel Yatosha kwa wadau wa Airtel jijini Mwanza, Meneja wa kampuni hiyo kanda
ya ziwa Ally Maswanya alisema" Tumeamua kushusha gharama hizo
kutokana na maagizoya mamlaka ya mawasiliano ambayo iliagiza gharama za simu kushushwa
kutoka hilingi 112 kwa dakika hadi
shilingi 34.92.
Kwa sasa huduma yaairtel yatosha ina punguzo la
hadi asilimia 88 na inalenga kurahisisha mawasiliano kwa wateja wa hali zote
kwa kuwawezesha kutumia kiwango kidogo cha fedha kupata muda wa maongezi wa
kuanzia dakika 10 kupiga mitandao yote ,meseji bila kikomo na huduma ya
internet".
Punguzo hilo la bei linatoa faraja kwa watumiaji
wa mtandao huo kwa kuwa litawawezesha kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho
walikuwa wakikitumia hapo awali. Aliongeza Maswanya.
Akiongea wakati wa halfa ya uzinduzi Mteja wa
Airtel na mkazi wa Mwanza Bi Agness Emmanuel alisema" Aritel yatosha
sasa ndio suluhisho la mawasiliano ya simu ya bei nafuu, tunashukuru Airtel kwa
kutoa vifurushi vingi na vya bei nafuu vinavyokidhi adha ya sisi wateja.
Huduma hii itatuletea urahisi wa mawasiliano
bila haja ya kuwa na simu nyingi na usumbufu wa kuwa na line nyingi. Kwakweli
Airtel yatosha itakuwa ni mkombozi katika mawasiliano.
Kwa upande wake Bwana Brighton Maisel moja
ya wateja waliohudhuria uzinduzi huo alisema"ni kwa muda mrefu sasa
mawasiliano ya simu za mkononi kwenda mitandao mingine yamekuwa ya gharama za
juu hivyo nashukuru sana serikali kuweka sheria ya kupunguza bei kati ya mitandaa
na Airtel kwa kutii na kuja na Airtel yatosha ambayo sasa inatuwezesha
kuwasiliano kwa bei nafuu na wateja wote wa mitandao ya simu za mkononi
mingine"
Airtel wiki hii pia bado itaendelea kufanya uzinduzi wa huduma hii katika mikoa
ya Morogoro, Mbeya, Arusha, Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa kuwafikia watanzania
na kuwaelimisha kuhusu huduma hii ya Airtel
Yatosha Kujiunga na huduma hii mteja anatakia kupiga *149*99# na
kuunganisha moja kwa moja kwenye orodha ya huduma hii na kuchagua kifurushi anachokipenda
na kuweza kujipatia dakika za maongezi, ujumbe mfupi na kifurushi cha internet.
0 comments:
Post a Comment