Richa Adhia akipokea zadi ya glasi kutoka kwa
mmoja wa mabalozi wa kinywaji cha Baileys kinachosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti
**** ****
Miss Tanzania 2007 Richa Adhia amewataka
watanzania kujenga utamaduni wa kuwakupenda na kuwajali watu wengine
wakiwemo wenye mahitaji maalum kama watoto na wazee kwa kuwa wanahitaji
faraja toka kwa jamii nzima nyakati zote badala ya kusubiri maadhimisho
ya sikukuu mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kilele cha msimu wa
siku ya wapenda nao ulioandalia na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji
cha Baileys katika viwanja vya shoppers jijini Dar es Salaam, Richa
alisema “siku ya wapendanao ikitumika kuongeza ari ya kuwasaidia watu
wenye mahitaji inakuwa na maana zaidi kuliko kuitumia siku hiyo kwa
mapenzi zaidi na sio vibaya kutumia siku ya wapendanao kuanzisha mapenzi
mapya au kuboresha mapenzi yaliyokuwepo lakini pia itumike kuwakumbuka wahitaji
ambao ni wazee na watoto”.
Kwa upande wake Meneja Masoko wa vinywaji vikali
kutoka Kampuni ya bia ya Serengeti Emilian Rwejuna amesema “ tumeamua kufanya
kampeni hii ili kuamsha ari ya kuwajali na kuwapenda wengine ikiwemo kujenga
utamaduni wa kuwanunulia zawadi kama tulivyofanya kwa wapenzi wa kinywaji cha
Baileys na kwa kuwa zawadi zina mchango mkubwa katika maisha ya mahusiano hivyo
mtoto anayempa zawadi mzazi wake hujiweka katika mazingira mazuri kimahusiano
kuliko asiyefanya hivyo”.
Pia alielezea kuwa Kampuni ya bia ya Serengeti
imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuhamasisha na kutoa chachu na kuahidi itaendelea
kuhamasisha mahusiano mema miongoni mwa jamii.
Kampeni ya msimu wa valentine
iliyoandaliwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha
Baileys ilinza tarehe mosi mwenzi wa Februari kwa kupita katika maeneo
mbalimbali ya manunuzi ili kuwahamasisha wananchi kujenga utamaduni wa
kuwanunulia wenzi wao zawadi na kukamalika siku ya wapendanao Februari 14.
Ambapo zawadi mbali mbali zilitolewa katika
kampeni hiyo ikiwemo chupa ya Baileys, fulana, glasi, maua na kubwa zaidi pea
nane zilipata bahati ya kupata chakula jioni katika mgahawa wa Akemi uliopo
jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment