Waziri Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana
na Mchungaji Trafaina Aseri Nkya ambaye pia ni msaidizi wa Askofu
Mteule wa Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria na ujumbe wake
walipofika nyumbani kwake eneo la Ngarashi kijijini kwake Monduli,
kumshukuru kwa harambee ya ujenzi wa kanisa lao aliyoiendesha Januari
mwaka jana na kupatikana kiasi cha shilingi millioni 200 zikiwa ni fedha
tasilimu pamoja na ahadi.
ujumbe wa
kamati ya ujenzi wa kanisa hilo ukimsikiliza Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasindikizawajumbe hao.
Waziri Mkuu
Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa, amewataka
vingozi wa dini nchini, kusaidia na kurejesha hali ya amani kati ya
wasilam na wakiristo ambayo inaonekana inaanza kupotea.
Akizungumza
hayo nyumbani kwake Monduli, wakati alipokuwa akipokea ujumbe kutoka
kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Lowassa
amesema vurugu na mauaji yaliyotokea huko Buserere, yanasikitisha sana
na kuongeza kuwa ni dalili mbaya ya kutoweka kwa amani ya Tanzania.
``Rais
ameelezea masikitiko yake, kwa kweli inasikitisha sana, mimi nawaomba
viongozi wa dini na madhehubu yote wasimamie na kuzuia mambo haya,
nawaomba watanzania wenzangu tusali kwa imani zetu kuomba amani yetu
isipotee`` alisema Lowassa kwa masikitikiko makubwa.
Katika fujo
hizo za Buserere,mchungaji mmoja wa kanisa la sabato aliuwawa baada ya
kuzuka kwa mapigano kati ya waislam na wakristo.Chanzo cha mapigano
hayo kilikuwa ni wakristo kuamua kuchinja ng'ombe na kuuza kwenye bucha
lao, hatua iliyopingwa na wananchi wa dini ya kiislam kwenye eneo hilo.
Ujumbe huo
uliyofika nyumbani kwa Mh Lowassa ukiongozwa na msaidizi wa askofu
mteule wa KKKT Dayosisi ya kusini mashariki mwa ziwa victoria, ulifika
kumshukuru kutokana na kusimamia na kuendesha harambee ya ujenzi wa
kanisa kuu la Shinyanga January mwaka jana ambapo zaidi ya shillingi
millioni 200 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana.
0 comments:
Post a Comment