Kufuatia changamoto ya muda mrefu ya
upatikanaji wa taarifa muhimu za hali ya hewa nchini, sasa Mamlaka ya
Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na kampuni ya Vodacom
Tanzania zimefanikisha kuwawezesha watanzania kuweza kupata taarifa
muhimu za hali ya hewa kwa njia ya haraka zaidi na rahisi.
Mfumo
huu maalumu utawezesha upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa kupitia
njia ya simu utasaidia kwa kiasi kikubwa na kutoa nafasi ya wahusika
kuchukua tahadhari pale inapobidi na pia kuweza umma kupanga shughuli
zao za kila siku.
Akizungumzia
mpango huo mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Dr.Agnes Kijazi, amesema kuwa Mamlaka hiyo inajitahidi kadri inavyoweza
kutumia fursa za kiteknolojia zilizopo ili kuweza kuhakikisha kuwa
watanzania wanapata taarifa za hali ya hewa za mara kwa mara pale
wanapohitaji.,
“Nchi
yetu ni kubwa sana na maeneo mengi yanatofautiana kwa hali ya hewa,
wakati mwingine nyenzo zinazotumika kutoa taarifa ya hali ya hewa
haziwafikii watu wote pale wanapokuwa, njia ya simu ni bora zaidi kwani
watu wengi wanatumia simu hivyo ni rahisi pia taarifa hizi kuwafikia
watu wengi zaidi, alisema Dr. Kijazi na kuongeza kuwa kuna watu ambao
wanasafiri kwa njia ya maji na anga ni muhimu sana watu hawa kupata
taarifa hizi za kabla ya kusafiri ili waweze kuchukua tahadhari.
itakuwa ni jambo jema sasa watanzania kupata taarifa hizi muda wote
wanapo hitaji,” alisema Dr. Kijazi.
“Tunayo
fursa nzuri ya kutumia maendeleo ya teknolojia kuhakikisha kuwa
tunawapatia watanzania uwezo wa kupata taarifa hizi za msingi,” Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom,
Kelvin Twissa amesema kuwa wanafuraha kuungana na Mamlaka ya Hali ya
Hewa Tanzania katika kuwapatia watanzania taarifa za hali ya hewa
kupitia njia ya simu, ikumbukwe pia TMA ndio chombo kilichopewa Mamlaka
ya kutoa taarifa za hali ya hewa nchini.
“Sekta
ya mawasiliano ya simu imekuwa kwa kiasi kikubwa sana kila mtu
anahitaji kuwa na mawasiliano ya simu changamoto ya upatikanaji wa
taarifa za hali ya hewa sasa itakuwa imetatuliwa kwa kiasi kikubwa,”
alisema Twissa na kuongeza kuwa, Vodacom tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa
kufikia wateja wengi zaidi kutokana miundombinu tuliyonayo. Tunatumia
mitambo yenye teknolojia ya juu na ninaamini kuwa katika maendelea ya
kiteknolojia Vodacom tumefanikiwa sana,” alisema Twissa.
“Sasa
tumeweza kuwafikia hadi wakazi wa kisiwa cha Gozba kisiwa ambacho kwa
muda mrefu kimekuwa hakina mawasiliano, wakazi wengi wa eneo hilo
wanajihushisha na shughuli za uvuvi kwa kuwawezesha wao kupata taarifa
za hali ya hewa kwa njia ya simu kutawasaidia sana.
“Wateja
wa Vodacom sasa wanaweza kupata taarifa hizi kwa njia rahisi sana kwa
kuandika neno Wthr na Mkoa anaotoka na kisha kutuma kwenda 15588, Mfano
mteja atatakiwa kuandika Neno Wthr Dar alafu watume kwenda 15588. Na
hapo watapokea ujumbe wa kukubaliwa kuunganishwa na huduma na kuanza
kupokea ujumbe wenye taarifa za hali ya hewa na kutozwa shilingi 100 kwa
kila ujumbe.
Alihitimisha
Twissa kwa kuwasihi watanzania kutumia fursa hii kupata taarifa za hali
ya hewa na kujijengea utamaduni wa kutafuta na kupata taarifa hizo ili
kuwa na tahadhari endapo kuna tatizo lolote linaweza kujitokeza Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji, Starfish Mobile East Africa Limited,
Rashma Bharmal Shariff, amesema kwa sasa teknolojia inayo mchango mkubwa
katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, na teknolojia ya simu
inaendelea kurahisisha mawasiliano kwa kufanya yawe yanapatikana kila
sehemu[z1] [z1] na kwa gharama nafuu.
Amesema
kuwa mikakati ya ushirika maridhawa, kama ushirika ulioundwa na TMA,
Vodacom Tanzania na Starfish Mobile, habari za uhakika zinaweza
kupatikana kwa urahisi na kwa haraka zaidi. Kwa mfano, wakulima wataweza
kupata taarifa [z2] [z2]za hali ya hewa, jambo ambalo ni muhimu ili kupata matokeo mazuri katika shughuli zao za kilimo.
0 comments:
Post a Comment