Nafasi Ya Matangazo

December 03, 2012


MWIMBAJI maarufu wa muziki  wa Injili nchini, Rose Muhando na mwenzake Enock Jonas (Zunguka) wanatarajiwa kuutikisa mji wa Bukoba  katika tamasha la kwanza kubwa kufanyika Mkoani Kagera.



Tamasha hilo litafanyika katika uwanja wa Kaitaba na baadae katika Ukumbi wa Lina’s siku ya tarehe 9 mwezi huu ambayo ni siku ya Uhuru wa Tanganyika.



Akizungumzia tamasha hilo Rose amesema amejiandaa kusherekea  Uhuru kwa aina yake tofauti na watu wengi walivvozoea kwa kuwashirikisha watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu.



Nimefurahi kupata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha hili la aina yake hasa katika  mkoa wa Kagera ambapo itakuwa mara ya kwanza kuonekana live katika mji wa Bukoba.



Nawaomba wananchi wa Bukoba kufika kwa wingi katika tamasha hili la kipekee katika ukuonyesha moyo wa upendo kushirikiana na kusaidia jamii ya watu wengine wasio jiweza.



“nimejiandaa kuwapa nyimbo mpya ambazo bado hawajawahi kuzisikia,itakuwa mara ya kwanza kuziimba katika tamasha hili.alisema



Tamasha hilo la Shangwe Kagera lina lengo la kuielimisha jamii na kuamsha mwamko wa kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika maisha magumu.



Wakati huohuo Enock Jonas 'Zunguka' wamewataka wakazi wa Kagera kukaa sawa kwa ajili ya tamasha hilo na watarajie kupata burudani ya kutosha na ya kipekee kutoka kwake  ambayo itawajenga roho ya imani, kupendana na kusaidia watu yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili nao waweze kufaraia maisha.



Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Beula Communications Ltd, ambao ni waandaji wa tamasha hilo,Melkizedeck Mutta anasema kuwa matayarisho ya tamasha hilo yanaendelea vizuri kutokana na mwitikio mkubwa wa watu mbalimbali waliojitokeza kushiriki.



Pia, Mutta anasema bendi ya muziki ya wazawa mkoa huo, Kakau Band pamoja na vikundi vingine vya wanakwaya  wa makanisa mbalimbali, kikundi cha watoto yatima wamejitokeza pia kutumbuiza.



 “Mpaka sasa tumekamilisha sehemu kubwa ya matayarisho hayo na tayari tiketi zimeanza kuuzwa katika maeneo yote ya mji wa Bukoba nje ya mji” alisema.



Lengo la Tamasha: 

Ni kuhamasisha jamii kuishi kwa amani,kupendana na kusaidia watu wengine hasa wasiojiweza kimaisha  ili na wao wajione ni sehemu yao.



Katika  kutambua hilo kampuni yetu iliamua kufanya utafiti mdogo nakugundua changamoto nyingi katika Mkoa wa Kagera, mojawapo ni kuwa na  watoto wengi wanaoishi katika mazingira magumu. Baada ya kuliona hili, tulitembelea vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao, mojawapo ni Tumaini Children’s Centre   kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Ki lutheri Tanzania (KKKT).



Kituo hiki kinalea watoto wote bila kujali kabila,jinsia wala dini zao,  kwa sasa kituo hiki kinahudumia watoto zaidi ya 800, kwa kuwapatia elimu,chakula, malazi n.k  ambapo kwa muda mrefu kimekuwa kikipata msaada toka Sweden ambao kwa sasa wametangaza kuusitisha kwa maelezo kuwa jamii ya Watanzania inapaswa kujifunza na kuanza kuhudumia watu wao wenyewe.

Posted by MROKI On Monday, December 03, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo