Kanisa
katoliki tanzania limepata pigo kwa kifo cha Mhashamu askofu Aloysius
Balina (pichani), Askofu wa Shinyanga, kilichotokea katika hospitali ya
Bugando jijini Mwanza tarehe 6 Novemba, 2012 saa tano asubuhi. Alikuwa
na saratani.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika Shinyanga Jumamosi tarehe 10 Novemba, 2012.
Mhashamu
askofu Aloysius Balina, alizaliwa Juni 21,1945, Ntuzu, Bariadi mkoani
Shinyanga, Upadre mwaka 1971 na alikuwa askofu mwanzilishi wa jimbno la
Geita mwaka 1985, na baadaye akateuliwa kuwa askofu wa Shinyanga mwaka
1997.
Kwa
zaidi ya miaka 20 amesimamia shughuli za kanisa Katoliki katika idara
ya afya, akiwa vile vile mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya rufaa ya
Bugando. Yeye ndiye mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Bugando.
Marehemu alizaliwa
Juni 21,1945, Ntuzu, Bariadi mkoani Shinyanga, Upadre mwaka 1971 na
alikuwa Askofu mwanzilishi wa jimbo la Geita mwaka 1985, na baadaye
akateuliwa kuwa askofu wa Shinyanga mwaka 1997.
Kwa
zaidi ya miaka 20 amesimamia shughuli za kanisa Katoliki katika idara
ya afya, akiwa vile vile mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya rufaa ya
Bugando. Yeye ndiye mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Bugando.
Mhashamu
askofu Aloysius Balina enzi za uhai wake akiwa na Rais Jakaya Kikwete
katika moja ya shughuli za Hopsitali ya Bugando, Mwanza
Mhashamu askofu Aloysius Balina enzi za uhai akihutubia
Mhashamu askofu Aloysius Balina akisalimiana na Laurean Kardinal Rugambwa enzi za uhai wao.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumanne, Novemba 6, 2012, amelitumia Kanisa Katoliki Tanzania salamu za
rambirambi kuomboleza kifo cha Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Mhashamu
Baba Askofu Aloysius Balina aliyefariki dunia majira ya saa tano asubuhi leo
kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza.
Katika
salamu zake za rambirambi kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mshahamu Baba
Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Rais Kikwete amesema: “Nimepokea kwa mshtuko mkubwa
taarifa za kifo cha Mhashamu Baba Askofu Aloysius Balina ambaye nimeambiwa
ameaga dunia asubuhi ya leo kwenye Hospitali ya Rufaa ya Buganda, Mwanza, kwa
ugonjwa wa kansa.”
Amesema
Rais Kikwete katika salamu zake hizo: “Mhashamu Baba Askofu Balina alikuwa
kiongozi hodari na mwadilifu ambaye siyo tu alichangia kipekee katika mwenendo mzuri
wa kiroho wa waumini wa Kanisa Katoliki bali pia katika maendeleo ya Watanzania
wote kwa jumla.”
“Kifo
chake kimetuondolea kiongozi mwema ambaye tutazikosa busara zake na uongozi
wake. Lakini napenda kukuhakishia Mshahamu Baba Askofu kuwa sisi ndani ya
Serikali tutaendelea kutambua na kuthamini mchango wa Askofu Balina alioutoa
kwa nchi yetu katika maisha yake,”
amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Baba
Askofu, nakuomba upokee salamu za rambirambi za Serikali ninayoiongoza na zangu
binafsi kufuatia msiba huu mkubwa. Aidha, kupitia kwako, naomba uwafikishie
salamu zangu viongozi na waumini wote wa Kanisa Katoliki kwa kuondokewa na
kiongozi na muumini mwenzao. Naungana nanyi kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa
Rehema, aiweka pema peponi roho ya Marehemu. Amen.”
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Novemba, 2012
0 comments:
Post a Comment