Meneja
Mawasiliano wa Airtel Kanda, Jackson Mbando (kulia) akimkabidhi kwa
Diwani wa Viti Maalum CCM, Vumilia Mwenda, Tarafa ya Kiponzero, Ifunda
Mkoani Iringa. Wanaoshuhudia makabidhian o hayo yaliyofanyika mwishoni
mwa wiki ni Katibu wa Mbunge wa Kalenga, Martin. Airttel ilitoa msaada
huo wa vitabu kwa shule nne za jimbo la Kalenga mkoani Iringa.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Lyandembela iliyopo Ifunda mkoani Iringa,
wakionesha vitabu vya masomo ya Sayansi na Hisabati vilivyogawiwa katika
Shule nne katika jimbo la Kalenga Mkoani Iringa mwishoni mwa wiki na
kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel.Kulia ni Diwani wa Viti Maalum
Vumilia Mwenda
Meneja
wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Beda Kinunda (kulia)
akimkabidhi vitabu vya masomo ya Sayansi Katibu wa Mbunge wa Kalenga,
Martin Simangwa Airtel ilitoa msaada huo wa vitabu kwa shule nne za
jimbo la Kalenga mkoani Iringa
Meneja
wa Airtel Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Beda Kinunda akizungumza mara
baada ya kukabidhi vitabu vya masomo ya Sayansi kwa shule nne Kiponzelo, Wasa, Mgawa and Lyandembelaza jimbo la Kalenga mkoani Iringa
******
· Shule 4 za sekondari mkoani Iringa za faidi na msaad huo
Katika
kuhakikisha kiwango cha elimu nchini kinainuka, kampuni ya simu za
mkononi ya Airtel chini ya mpango wake wa Shule yetu imeendelea kutoa
msaada wa vitabu kwa shule mbalimbali za sekondari ambapo mwisho mwa
wiki hii Airtel ilitoa vitabu kwa shule za sekondari Kiponzelo, Wasa,
Mgawa and Lyandembela zilizoko mkoani Iring.
Akiongea
wakati wa halfa ya kukabidhi vitabu iliyofanyika katika shule ya
sekondari lyandembela Diwani wa Viti Maalum CCM, Vumilia Mwenda, Tarafa
ya Kiponzero, Ifunda Mkoani Iringa alisema “Tunashukuru Airtel kwa kutoa
haki sawa kwa shule zote nchini kwa kuchangua shule kupitia droo ambayo
imeweza kuwafikia wanafunzi wa shule za Iringa hadi vijijini.
Tumefurahi sana kupata vitabu mbalimbali kwani shule ya sekondari za
hapa Ifunda zina changamoto ya upungufu wa vitabu hasa vya sayansi na
kulifanya somo hilo kuwa na wanafunzi wa chache, lakini hivi sasa
kutokana na msaada wa vitabu vilivyo tolewa vitaongeza ufaulu kwa
wanafunzi wetu”.
Nachukua
fulsa hii kuwaasa wanafunzi wavitumie vitabu hivi vizuri na kujiunga na
masomo ya sayansi, tunaamini vitabu hivi vitaleta ufanisi pamoja na kuwa
na changamoto ya walimu naahidi kuwashirikisha wizara ya elimu ili
kuongeza idadi ya walimu wa sayansi na kuongeza ufaulu zaidi” aliongeza
Bi Mwenda
Naye Mwalimu mkuu wa sekondari ya Wasa David Mpalanzi Iliyoko Wilaya Mfindi Mkoa wa Iringa akiongea kwa niaba ya wakuu wa sekondari wa shule za Mgama, Lyandembela and Kiponzelo alitoa
shukurani kwa Airtel na kusema msaada huo wa vitabu utaweza kuwa saidia
wanafunzi kuwa na uweza wa kujisomea zaidi na kuwawezesha kufaulu hadi
kwenda chuo kikuu ,kwani hapo awali kulikuwa na changamoto kubwa katika
shule zetu ambapo uwiano ulikuwa kitabu kimoja wanafunzi 15 hadi 20.
Lakini msaada huu utapunguza zaidi, kwa kweli huu ni msaada mkubwa
katika kuboresha taaluma na kuinua ufaulu hivyo tunaomba program hii ya
shule yetu iendelee ili kuwafikiwa watu wengi zaidi
Tunaomba
Airtel muongeze wigo wa kutoa misaada mbalimbali ya kuboresha elimu na
mazingira kwa ujumla ikiwemo , kutoa komputa, kusaidia upatikanaji wa
maji, na mengine mengi. Akiongea kwa niaba ya wanafunzi Kaka Mkuu wa shule ya Lyandembela sekondari Taifa Malata ametoa
shukurani kwa niaba ya wenzao huku akibainisha wanafunzi wengi walikuwa
wakifeli katika masomo mbali mbali kutokana na ukosefu wa vitabu
,wanafunzi hao wameomba uongozi wa Airtel kuwafikirili kutatua
changamoto zingine kama ukosefu wa maji, pamoja na kuwajengea maktaba ya
kuwatosheleza ili kujisomea kwa nafasi zaidi
Akiongea
kwa niaba ya Airtel Meneja mauzo wa Airtel Beda Kinunda amewataka
wanafunzi wa sekondari zote mkoani Iringa kuongeza uwezo wa kujisomea
ili Airtel ione ufaulu wa wanafunzi unaongezeka kupitia msaada unatolewa
na Airtel, pia natoa wito vitabu hivi vitunzwe ili viweze kuwafaidisha
wanafunzi wengi kwa kuwa Airtel imeanzisha mpango wa Airtel Shule yetu
ili iwe chachu kukuza Elimu.
Airtel
imeanzisha mpango wa Airtel Shule yetu ili kuendeleza Elimu Inchini
Tanzania Umeanzisha Mpango huo na kuweza kushindanisha shule mbalimbali
zaidi shule 3000 na shule zinazo shinda hupewa vitabu katika bahati na
sibu hiyo. shule NNE za mkoa wa Iringa zilibahatika kushinda.
0 comments:
Post a Comment